Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwaonya maafisa ardhi na
maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya
ardhi nchini wakati wa uzinduzi Master Plan ya mji wa Iringa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi kitabu cha Master
Plan ya mji wa Iringa Meya wa Halmashauri ya Iringa Alex Kimbe.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Meya wa
Halmashauri ya Iringa Alex Kimbe na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini
Mchungaji Peter Msigwa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipongezwa na Mbunge wa jimbo
la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa mara baada ya Uzinduzi wa Master
Plan ya mji wa Iringa.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Iringa waliofika kushuhudia Uzinduzi huo.
……………………………………………………………………………………….
Na Hassan Mabuye Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewaonya maafisa ardhi na
maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya
ardhi nchini.
Waziri Lukuvi aliyasema hayo leo katika ukumbi wa shule ya sekondari Lugalo mjini Iringa wakati wa Uzinduzi wa Master Plan ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Amesema mchezo huo wa ufisadi
ambao umekuwa ukitumiwa miaka yote na maofisa ardhi nchini ameubaini
na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutokubaliana na ramani za
maeneo mapya zinazoletwa na wataalam hao bila ya wao kufika maeneo
husika na kuoneshwa maeneo hayo ili kujiridhisha.
Waziri Lukuvi amefichua kuwa
ufisadi unaofanywa na maafisa ardhi nchini kwa kupima viwanja hewa kwa
ajili ya maslahi yao na kusema kuwa mbinu ambayo wamekuwa wakiitumia
kuiibia serikali amekwisha ibaini na hata kubali kuona mbinu hiyo
inapewa nafasi katika serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt
John Pombe Magufuli .
Maafisa ardhi wakishirikiana na
maafisa mipango miji pamoja na wapima wamekuwa wakitajirika sana
kwenye idara zao na wanatakata kwa ujanjaujanja na ufisadi
wanaoufanya kwa kutengeneza ramani zinazoonesha maeneo mazuri na muhimu
katika miji kwamba hayafai kutumika, kumbe wameyauza maeneo hayo kwa
mlango wa nyuma na kwa bei za juu.
Unakuta kwenye ramani
inayonyesha kuna bonde kubwa lisilofaa kujengwa kumbe ukifuatilia
eneo hilo ni zuri kuliko yote na hapo wametenga viwanja vya
kuuza. Unakuta ukipima kuna viwanja vingi na vizuri ambavyo ni vyao
wao wanachofanya baada ya kuuza viwanja halali za Halmashauri
hurudi kupima maeneo hayo walioonyesha ni mabonde na kugawana wao kwa
ajili ya kuuza kwa faida yao.
Lukuvi amesema kuwa
wathamini nao pi wamekuwa wakiwapunja wananchi wasio elewa kwa
kuwafanyia tathimini kubwa zaidi ya uhalisia wake na pindi pesa
inapotoka utakuta nyumba inathamani ya milioni 7 wakati wao wanasema
inathamani ya milioni 20 ili cha juu wapate wao.
“wakati nilipokuwa Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam niliweza kubaini ujanja wa wathamini baada ya eneo
ambalo nyumba zake zina thamani kati ya milioni 20 hadi 50 kwa maana
nyumba hizo ni za udongo ila maofisa hao walimtafuta mtu na
kutafuta nyumba nzuri zaidi na kumshikisha kibao kisha kumpiga picha
na kuandika kuwa nyumba hiyo inathamani ya zaidi ya milioni 200.
Niliamua kufanya uchunguzi wangu
na kumtafuta mtu aliyekwenye picha na kumbana ndipo aliniambia ukweli
kuwa mthamini huyo ni ndugu yake hivyo walikubaliana pesa ikitoka
atalipwa milioni 70 na milioni 130 ni za afisa huyo”
Hata hivyo alisema kuwa ujenzi
holela katika miji na halmashauri imesababishwa na ukilitimba wa utoaji
wa vibali kwa wakati na ndio sababu ya wananchi kuvamia maeneo yasiyo
pimwa japo kuanzia sasa wote waliopo katika maeneo yasiyo pimwa
watapewa leseni ya makazi ya miaka mitano na watalipa kodi ya ardhi
na baada ya miaka mitano wahakikishe wamepimiwa ili kupewa hati.
Hivyo Lukuvi aliwataka maafisa
ardhi na wathamini wa ardhi manispaa ya Iringa kutofanya kama maeneo
mengine kwa kufuata mpango maeneo yote ambayo yameelekezwa kwenye
Masta Plan hiyo na kwenda kutenda haki.
Katika hatua nyingine waziri
Lukuvi alitoa agizo kwa wale wote waliopewa ardhi kwa ajili ya
ujenzi wa hoteli na viwanda na wale waliouziwa viwanda vya serikali,
hotel na mashamba ya serikali kuviendeleza haraka kabla ya ardhi hiyo
haijapokonywa .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Bibi Amina Masenza akimkaribisha waziri Lukuvi amesema kuwa mkoa wa
Iringa umeendelea kuhamasisha wananchi kuzingatia sheria na
taratibu za ujenzi na kuachana na ujenzi holela na ndio sababu ya
kuja na Masta Plan hiyo ambayo imeanzishwa na aliyekuwa mstahiki meya
wa halmashauri hiyo Amani Mwamwindi.
Akitoa taarifa ya uandaaji wa
Masta Plan hiyo kwa ajili ya mwaka 2015-2035 Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Iringa Dkt William Mafwere, alisema kuwa dhumuni la
mpango huo ni kutatua changamoto zilizokuwa zinaikabili Manispaa na kuwa
dhana kuu ya mpango huo ni dhana unganishi ikijumuisha dhana nyingine.
Alisema jumla ya miradi 31
itatekelezwa katika awamu ya kwanza 2015-2020 kuwa baadhi ya miradi hiyo
ni kituo cha mabasi Igumbilo, kituo hicho kimeanza ujenzi na hatua ya
utekelezaji imefikia asilimia 30.
Nae Mbunge wa jimbo la Iringa
mjini Mchungaji Peter Msigwa alisema kuwa kazi inayofanywa na Waziri
Lukuvi ni tofauti na mawaziri wengine kwani amekuwa ni waziri wa mfano
katika kuchapa kazi.
“Kwa mnaonifahamu vizuri mimi
sio mbunge wa kusifia sifia ni mbunge mwenye msimamo ila nampongeza
sana Waziri Lukuvi ni waziri mchapakazi na kazi zake zinaonekana na
ndio maana hata bungeni ni waziri pekee ambaye bajeti yake ilipitishwa
kwa kishindo hata na sisi wabunge wa kambi ya upinzani”
Mpango Kabambe ni chombo cha
kuchochea utumiaji wa fursa zilizopo katika mji, kuongeza kasi ya
upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kupunguza na kumaliza migogoro ya
ardhi. kudhibiti ujenzi holela mijini na hutumika pia kuongoza,
kusimamia na kudhibiti ukuaji na uendelezaji wa mji na kutoa uhakika kwa
wawekezaji katika Halmashauri za Manispaa ya husika.
Tags
ARDHI