Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy
Mwalimu, viongozi na wadau wa tiba Asili na tiba Mbadala wakati wa
uzinduzi wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba
mbadala uliofanyika leo katika viunga vya ofisi ndogo za Wizara ya Afya
jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Shastri
Herbals Namdeo Shastri akionesha cheti cha usajili alichopewa leo
wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba mbadala
uliofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa kampuni yakimataifa
ya Cornwell Quality Tool & Chemicals Bi. Elizabeth Lema akipokea
cheti cha usajili cha Tiba Asilia na Tiba Mbadala kutoka kwa Waziri wa
Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba mbadala.
Wadau wa tiba Asili na tiba
Mbadala wakifuatilia kwa umakini hotuba ya uzinduzi wa mpango mkakati wa
Tiba asili na Tiba mbadala uliofanywa na Mh. Ummy Mwalimu katika ofisi
ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikata Utepe kuashiria
uzinduzi wa Mpango mkakati wa Tiba asili na Tiba mbadala, kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala Wizara ya Afya Dkt.
Edmund Kayombo, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Otilia
Gowele na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba asili na Tiba
Mbadala Dkt. Muhame.
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa
Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba mbadala,
Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Otilia Gowele na kulia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala Wizara ya Afya Dkt.
Edmund Kayombo.
……………………………………………………………………
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepiga marufuku watoa
huduma za tiba asili na tiba mbadala kutangaza dawa za asili ambazo
hazijasajiliwa na Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala kisheria.
Hayo amezungumza leo jijini Dar
es salaam wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba
mbadala ili kuweza kuwaongoza watoa huduma za tiba asili kuweza kutoa
huduma bora na salama kwa watanzania wanaotumia tiba hizo.
“Dawa zote za asili
zinazotengenezwa na watoa huduma za asili lazima zisajiliwe na baraza
husika kwa mujibu wa sheria ili kupata usalama wa matumizi kwa
watanzania na marufuku kwa watoa huduma wa tiba asili kutangaza dawa
hizo kama hazijasajiliwa” alisisitiza Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala wanawajibu wa kuwa na sehemu
maalum ya kutengenezea dawa zao na mahali pakutolea huduma zao ili
kutowachanganya wateja wao wanapohitaji tiba asilia.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema
kuwa pindi watoa huduma ya tiba asili na tiba mbadala wanaposajili dawa
zao zitaongeza chachu ya kutengeneza viwanda vya dawa hizo ili kusapoti
juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala Wizara ya Afya Dkt. Edmund Kayombo
amesema kuwa dawa za tiba asili zinatakiwa kusajiliwa ili kuweza
kutambua na kuweka usalama kwa watumiaji wa dawa hizo.
Aidha Dkt. Kayombo amesema kuwa
umuhimu wa kusajili dawa hizo ni kuwasaidia watoa huduma za tiba asili
na tiba mbadala kuweza kupata soko kimataifa na kutangaza bidhaa za
Tanzania nchi za nje ili kuongeza ushindani wa biashara.
Kwa upande wake mtoa huduma za
tiba asili na tiba mbadala Bi. Elizabeth Lema amesema kuwa wanapaswa
kusajili dawa zao ili kuwathibitishia ubora na usalama watumiaji wa dawa
za tiba asili na tiba mbadala nchini.
Tags
AFYA