Na Unique Maringo
WAKILI wa Serikali Estazia Wilson ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi katika kesi
ya kutakatisha fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange `Kaburu` kuwa upelelezi unaendelea na kwamba kuna nyaraka mbalimbali zimepelekwa kwa mtaalamu wa maandishi.
ya kutakatisha fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange `Kaburu` kuwa upelelezi unaendelea na kwamba kuna nyaraka mbalimbali zimepelekwa kwa mtaalamu wa maandishi.
Alidai kuwa shauri hilo limekuja kwaajili ya kutanjwa ambapo wanasubiri ripoti ya polisi.
Wakili upande wa utetezi Evidius Mtawala aliomba tarehe ya karibu ili upande wa mashtaka uweze kukamilisha upelelezi huo.
Hakimu Mkazi Mkuu,
Victoria Nongwa aliutaka upande wa jamuhuri kujitahidi kuharakisha
upelelezi kwasababu washtakiwa wapo ndani na kwamba wajitahidi
kufuatilia ripoti hiyo.
Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 8 mwaka huu kwaajili ya kutanjwa.
Evans Elieza Aveva na
makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi,
kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.
Katika shtaka la
kwanza, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu
ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba
inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.
Katika shtaka la pili
alidai kuwa Machi 15,2016 katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe
Ilala Aveva akijua alitoa nyaraka za uongo ambayo ni fomu ya maombi ya
kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakati akijua ni kosa.
Katika la tatu la
kutakatisha fedha, Aveva na Nyange wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15 na
Juni 29,2016 Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha
fedha kwa kupata USD 300,000 wakati wakijua ni zao la uhalifu.
Kwa upande wa shtaka
la nne la kutakatisha fedha,Aveva anadaiwa kuwa kati ya Machi 15,2016
katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 300,000 wakati akijua
zimetokana na kughushi.
Katika shtaka la tano
la kutakatisha fedha, mshtakiwa Nyange anadaiwa kuwa Machi 15,2016
katika benki ya Baclays tawi la Mikocheni alimsaidiaAveva kujipatia USD
300,000 wakati akijua fedha hizo zimetokana na kughushi.
Washtakiwa wapo rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana.