Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC), Prof. Mohammed Janab ameieleza
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 30, 2017 kuwa moyo wa
Mfanyiabiashara Yusuf Manji umewekwa vyuma ili kumsaidia kupumua.

Prof. Janab ambaye ni Daktari wa
moyo na Shahidi wa kwanza upande wa uetetezi ameyasema hayo mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa ushahidi katika kesi
ya dawa za kulevya inayomkabili Manji ambapo akiongozwa na Wakili wa
utetezi, Hajra Mungula, alisema yeye ni Daktari wa moyo wa Taasisi ya
JKIC.
Amesema anamfahamu Manji baada
ya kufikishwa katika Taasisi hiyo February 2017 akiwa mwenye matatizo ya
moyo na kuongeza kuwa alipofikishwa hapo alifanyiwa vipimo na jopo la
madaktari lililobaini Moyo wake umewekewa vyuma ambapo akaingizwa mipira
maalum na kubaini kwamba upo katika hali nzuri.
”July 2017 alirudishwa tena
katika Taasisi yetu akiwa na tatizo hilo la moyo pamoja na maumivu ya
mgongo na kutokuwa na usingizi.”
Prof. Janab amesema alivyorudi
hapo walimpokea kama mgonjwa aliyetibiwa nje ya nchi na ripoti
ilionyesha ametibiwa Florida, Marekani.
Alipoulizwa na Wakili Mungula
kama mgonjwa aliyewekewa vyuma katika moyo anaweza kutumia dawa za
kulevya, Prof. Janab alijibu kwamba huwa haruhusiwi kufanya baadhi ya
mambo ikiwemo kuvuta sigara, kutumia Heroin.>>>”Hivyo kama
akitumia athari zake ni kwamba mirija ya moyo itaziba, kisha atatakiwa
afanyiwe upasuaji mkubwa zaidi.”
Prof. Janab ameongeza kuwa
katika awamu ya pili ya Manji kurudi hospitalini hapo walimsaidia
kumtibia maumivu aliyokuwa nayo kwa kumpa Drip ya Paracetamol’s na
Sindano ya Tram a do.
Akijibu hoja ya Wakili wa
Serikali, Timony Vitalis kwamba matumizi ya dawa za kulevya yanaweza
kusababisha ugonjwa wa moyo, Prof. Janab alijibu ndio.
Kesi imeahirishwa hadi August 31, 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
Tags
Yussuf Manji