| Wakimbiza mwenge Kitaifa wakikagua Soko la Namonge. |
| Soko la Mazao la Namonge |
| Kiongozi wa mbio za mwenge akikagua baadhi ya mabanda kwenye Soko la nafaka la Namonge. |
| Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akionesha eneo la ukuta wa Ghara kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru. |
| Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Amour Hamad Amour akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya Bukombe Chacha Moseti. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Amour Hamad Amour Akizindua Soko la Mazao baada ya kuwa ametoa maelekezo ya ukarabati wa soko hilo.
PICHA NA JOEL MADUKA(MADUKA ONLINE)
|
Kiongozi wa
mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour
Hamad Amour amesikitishwa na Ujenzi wa mradi wa soko la Mazao Namonge lililopo wilayani Bukombe Mkoani Geita kwa kujengwa chini ya kiwango na hali ambayo
imepelekea kuwepo kwa nyufa nyingi kwenye maeneo mengi ya jingo hilo.
mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour
Hamad Amour amesikitishwa na Ujenzi wa mradi wa soko la Mazao Namonge lililopo wilayani Bukombe Mkoani Geita kwa kujengwa chini ya kiwango na hali ambayo
imepelekea kuwepo kwa nyufa nyingi kwenye maeneo mengi ya jingo hilo.
Na pia amemtaka mkandarasi kurekebisha haraka
iwezekanavyo kabla ya mwenge wa uhuru kuondoka Mkoani humo huku akimpa siku
mbili maeneo yote ambayo yananyufa kufanyiwa ukarabati haraka zaidi.
Kiongozi
huyo wa mwenge ameendelea kuwasisitiza viongozi
wa halmashauri kuhakikisha wakandarasi wanakuwepo katika miradi
inayozinduliwa,kuwekewa jiwe la msingi na kutembelewa na mwenge wa uhuru ili
kujibu changamoto zitokanazo na miradi hiyo.
Mhandisi wa
ujenzi wa halmashauri hiyo CHACHA MOSETI ametoa taarifa
ya mradi huo kwa mwenge na gharama
Sh,581,217,690 hadi kukamilika kwake ambapo Sh,552,156,805.5 ni Fedha za
serikali kuu kupitia mpango wa market insfrastructure,value addition and Rural
Finance na Sh,29,060.884.5 ni mchango wa Halmashauri.
Aidha mpaka
sasa jumla ya fedha zilizotumika ni Sh ,552,156.805.5 ambazo ni fedha za
serikali kuu.
Hata hivyo Baada
ya kukagua maeneo mbalimbali ya soko hilo na kujionea ujenzi huo Kiongozi wa mbio za
mwenge wa uhuru kitaifa AMOUR HAMAD AMOUR akatoa maagizo.
“Baada ya
kukagua mradi huu tumeona mapungufu mengi mradi umepasuka kwenye kuta sasa kwa
vile mradi huu umekusudiwa kuwekewa jiwe la msingi na tumemuuliza mkanadarsi
hayupo eneo husika wakandarasi wanatakiwa kuwepo kwenye mradi ili kujibu
maswali ambayo yatakuwa yakiulizwa Tunamuomba mkandarasi kabla ya risala ya
utii kwa
Mheshimiwa Rais awe amefika uwanjano na tunatoa siku mbili awe
amekamilisha ukarabati wa kasoro ambazo tumezikuta “Alisisitiza Hamad.
Wafanyabiashara
wa zao hilo Mlalu Bundala na Emmanuel Mhuli Kasuku wamezungumzia umuhimu wa
soko hilo litakapokamilika kuwa
litawasaidia kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya zao
ambalo wanalilima.
Kauli mbiu
ya mwenge huu ni “Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi
yetu.”
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Tags
Mbio za Mwenge