Na Sales Malula
Mwimbaji
wa nyimbo za injili John lisu pamoja no waimbaji wengine wa nyimbo za
injili wanatarajia kupamba tamasha kubwa la uamsho linaloanza kesho.
Katika
mahojiano maalumu na Mtandao huu Mchungaji kiongozi wa Kanisa la
Tanzania Assemblies Of God (victory Christian center) DK. Huruma Nkone
amesema wameandaa mkutano wa uamsho unaoshirikisha watu wote bila kujali
utofauti wa madhehebu hayo
Akifafananua
zaidi alisema mnenaji katika mkutano huo wa uamsho ni mhubiri maarufu
hapa nchini Askofu Yona Suleiman kutoka kiomboi mkoani Singida.
Mkutano
huo wa uamsho utafanyika katika ukumbi Wa Kanisa la Victory Christian
Center Mbezi A mwai kibaki road ambapo usafiri wa kuja Kanisani
utatolewa bure kuanzia Mwenge ambapo kwa tegeta na Bunju pia usafiri
utakuwepo.
Mkutano
huo wa siku tatu yaani tarehe1-3 September 2017 saa kumi kila siku
unatarajiwa kuwa wa Baraka ambapo wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam
watahubiriwa na kuacha Maovu
Ni
Kwa Neema Tu: Waimbaji wengine watakaopamba mkutano huo wa uamsho ni
Rivers of Joy International Kwaya ya Kanisa la KLPT Tageta na nyingine
nyingi.
DK Nkone ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar kujitokeza kwa wingi kwani Huduma ya maombi na maombezi itatolewa bure.
Tags
LISU