OFISI
YA MKURUGENZI
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imetenga eneo la
Makole D-Center lililoko katikati ya Mji wa Dodoma kuwa eneo rasmi kwa ajili ya
wafanyabiashara ndogo maarufu kama Machinga kufanya biashara zao badala ya
kupaga bidhaa ovyo mitaani hali inayopelekea kuharibu taswira ya mji.
Hatua hiyo pia itasaidia kuendana na kasi kubwa ya
ongezeko la wafanyabiashara hao kuingia Mjini humo kutoka mikoa mbalimbali
nchini tangu Serikali ilipohamia rasmi Dodoma ambako ni Makao Makuu ya Nchi.
Akizugumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani la
kufunga wa fedha uliopita lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Manispaa hiyo, Mkurugenzi wa
Manispaa ya Dodoma Godwin aliyewajulisha wajumbe na wananchi kuwa, sasa
Manispaa iko katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa miundombinu muhimu katika eneo hilo ikiwemo
vyoo ili shughuli za biashara zifanyike katika mazingira salama na rafiki.
“Tunatarajia eneo hilo litakuwa tayari kufikia
mwisho wa mwezi Agosti au mwanzo wa mwezi Septemba mwaka huu mara moja tutaanza
zoezi la kuwahamishia wafanyabiashara hao pale” alifafanua.
Alisema Manispaa inashirikiana kwa karibu na
viongozi wa wafanyabiashara hao katika zoezi hilo, na kwamba endapo eneo hilo
halitatosha, wafanyabiashara wengine watahamishiwa katika eneo la Chaduru .
Tayari Manispaa ya Dodoma ilishaanza zoezi la
kuwaondoa wafanyabiashara wa Matunda na chakula katika maeneo yasiyo rasmi na
kuwahamishia katika maeneo rasmi ya masoko ikiwemo soko la Sabasaba, Bonanza,
na Tambukareli.
MWISHO