Na.AngelaMsimbira
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa Mhe Seleman Jafo amemwagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kumrudisha Mkandarasi na Mtaalam
mshauri waliojenga mradi wa maji kijiji cha Itiso kilichopo Wilayani Chamwino kutokana
na kujenga mradi huo kinyume na mkataba uliotolewa na Serikali na chini ya
kiwango.
Mhe.
Jafo Ametoa agizo hilo wakati alipotembelea Mradi wa Maji wa Itiso uliokuwa ukisimamiwa
na Kampuni ya Audancia kwa kusimamiwa na Mtaalam Mshauri O&A Company Limited
uliogharimu kiasi cha shilingi 338,676,323
Mhe.
Jafo amesema kuwa Mkandarasi pamoja na mshauri wameondoka kwenye mradi kabla mradi
kukamilika kitendo ambacho kinaisababishia hasara serikali ambapo fedha ambazo zilitakiwa
kutumika kukidhi mahitaji ya wananchi zinapotea.
Mhe
Jafo amesema hajaridhika na kazi iliyofanywa na Mkandarasi Audancia aliyejenga mradi
wa maji kijijini Itiso kutokanana kulaza mabomba yaliyo chini
ya kiwango na ni kinyume na mkataba aliopewa na Serikali.
“Nimesikitishwa
na Mkandarasi wa Mradi wa Maji Itiso kwa kuwa amelaza mabomba yaliyo chini ya
kiwango tofauti na mkataba aliopewa na Serikali na kusababisha wananchi wa
kijiji cha Itiso kukosa kupata maji kwa wakati na kurudisha nyuma juhudi za
serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi
Amesema
Serikali imekuwa ikiwekeza fedha nyingi ili iweze kutekeleza miradi ambayo
itasaidia wananchi lakini miradi mingi hujengwa chini ya kiwango na kutokamilika
kwa wakati na hivyo kurudisha nyuma maendeleo kwa wananchi.
“Serikali
imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kujenga miradi ya maji lakini miradi mingi
imekuwa haikamiliki kwa wakati na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wananchi
kuwa serikali haitimizi ahadi zake“ Amesema
Amewaagiza
watumishi waliopewa dhamana yakusimamia miradi ya maendeleo kuhakikisha wanatumia
weledi wa kazi yao kuhakikisha miradi yote ya Serikali
inamalizika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa na waache kufanya kazi kwa mazoea.
“Watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia Miradi ya Maendeleo wanatakiwa kutimiza
wajibu wao katika kuleta maendeleo kwa wananchi”
Akisoma
taarifa ya Mradi wa Maji Itiso Fundi Sanifu
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Stephen Mzuri amesema Mradi wa maji Kijiji
cha Itiso ulianza kujengwa mwaka 2013 na kukamilika mwaka 2014 na kujengwa na Kampuni
ya Audancia kwa kusimamiwa na Mtaalam Mshauri O&A Company L.T.D uliogharimu
shilingi milioni 338,676,323/=
Amesema
kuwa kulingana na mkataba Mkandarasi alitakiwa kulaza mabomba ya Class C kwenye
laini inayotoa maji kwenye kisima na kupeleka kwenye tanki lakini mkandarasi alilaza
mabomba ya class B. Pia kuvuja kwa maji na vichoteo viwili kati ya vichoteo nane
havikuwa vinatoa maji.
Bw.Mzuri
amesema mpaka sasa vichoteo vitano kati ya kumi vinatoa huduma ya maji kijijini
na vichoteo vilivyosalia vinaendelea kufanyiwa marekebisho vitakapokamilika mradi
utahudumia watu zaidi ya wananchi 6000.
Aidha,
Mbunge wa Chilonwa Mhe.Joel Mwaka amempongeza Naibu Waziri kwa kutembelea kijiji
cha Itiso na kuangalia mradi wa maji uliokuwa ukisuasua tangu mwaka 2013 na kusababisha
wananchi kutokupata maji katika kijiji cha Itizo kwa muda mrefu.
Tags
Waziri Jaffo