LINDI: KUTOKANA na Tangazo la Serikali la mwaka 2017/2018 limetoa agizo la mkaa kutozidi ujazo wa kg 50.

Akitoa ufafanuzi kuhusu Tangazo hilo la mwaka huu kwenye maonyesho ya kitaifa nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Lindi Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Glory Mziray amesema agizo hilo linalenga kukidhi sheria ya mamlaka ya Vipimo ambayo vinataka mkaa kuwekwa katika kifaa au kibebeo kisichozidi ujazo wa kilo 50.
Glory alisema katika Tangazo hilo Vitanda vimepungua ambapo bei ya ushuru ilikuwa sh.120,000 kwa mwaka uliopita mpaka sh 20,000 mwaka huu na mlango toka sh. 90,000 mwaka jana mpaka sh.50,000 mwaka huu.
Alisema ufafanuzi huyo huu unapatikana katika ofisi zote za TFS au kwenye Tovuti na mitandao ya jamii ya TFS.
Akizungumzia Hifadhi za Misitu ya asili alisemawakala wa Huduma za Misitu inazo hifadhi za misitu asilia 12 amabazo zina vivutio ndwele na vingi vinapatikana katika maeneo hayo tu .
Alisema vivutio hivyo vinafaa kwa Utalii Ikolojia na Utalii Burudani ambapo TFS inajipanga kuuutangaza na kuutumia ipasavyo kwa faida ya Tanzania.
Glory alisema Serikali ya awamu ya tano imejikita katika kuimarisha Viwanda na Biashara katika kuhakikisha inakamilisha mpango huo wakala wa Huduma za Misituumeainisha viwanda 630 vinavyotumia malighafi ya miti ya serikali na Misitu ya asili, viwanda hivyo ni vidogo, vya kati na vikubwa viwanda hivyo vimetoa ajira kwa watu 13,150 wakati sekta ya misitu kwaujumlakwa zaidi ya wananchi milioni 3.
Kutojana na faida hizo Serikali imepiga marufuku usafirishaji wa magogo nje ya nchi isipokuwa nguzo zilizotibiwa (treated poles).
Akizungumzia kasi ya upandaji miti alisema haiendi sambamba na kasi ya ukataji miti.
Alisema miti zaidi ya 1000 hukatwa kwa siku na kueleza kuwa Tanzania hukata Mita za ujazo milioni 19 zaidi ya kiwango kiichoruhusiwa kwa mwaka kwa hali hiyo inalazimisha upandaji miti ufanyike kwa kasi kubwa ili kupunguza kiwango haramu cha ukataji Miti.
“Wakala wa Huduma za Misitu hupanda miti milioni mbili katika takribani hekta elfu 10 kwa mwaka hii huenda sambamba na agizo la serikali ambapo limeitaka kila wilaya kupanda miti Milioni 1.5 kwa mwaka”alieleza Glory.
Akizungumzia mazao ya asali alisema Wakala wa Huduma za Misitu ilikusanya Sampuli 63 za asali na kuzipeleka katika maabara za kimataifaambapo zote zilikidhi viwango vya masoko ya kimataifa .
Alisema hatua hiyo ya kupima asali ya Tanzania ni kuimarisha masoko ya asali inayozalishwa na wafugaji nyuki wa Tanzania.
“ Wakala wa Huduma za Misitu wanasimamia manzuki 82 na inatoa elimu kwa wafugaji mbalimbali wanaohitaji.
“Wakala umejiunga na mfumo wa serikali wa Ukusanyaji maduhuli kama alivyoagiza rais wa awamu ya Tano Mhe. John pombe Magufuli na maeneo yote ya TFS nchi nzima wameshaaanza utekelezaji na mafanikio yameanza kuonekana.
Alisema kuna mfuko wa misitu bapo unasaidia wananchi wanaofanya shughuli za uhifadhi na elimu ya ufugaji nyuki na upandaji Miti katika maeneo yote hapa nchini. wakala wa Huduma za misitu wana maoisa kila wilaya ili kuttoa huduma hizo.

Tags
MKAA