BANDA MEDIA BLOG

BUNGE NANENANE NI MAPACHA



DODOMA: BUNGE limesema kuwa hakuna jinsi yoyote ambayo muhimili huo unaweza kujitenga katika kushiriki katika maonesho ya wakulima Nanenane kwani sera na sheria za kilimo zinatungwa bungeni.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa habari wa Bunge,Patson Asumwisye Sobha alipokuwa akitoa maelezo ya shughuli za Bunge kwa Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk.Charles Tzeba wakati akitembelea mabanda malimbali kwenye naonesho ya Nanenane yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni manispaa ya Dodoma.

Patson alisema Bunge ni sehemu kubwa ya maonesho ya nanenane kwani sera ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi pamoja na sheria zake ni lazima mchakato upitie bungeni.

“Hakuna jinsi ambavyo Bunge linaweza kujitenga na Maonesho ya Nane nane kwani sera zote za Kilimo,Mifugo na Uvuvi zinapitia Bungeni.
“Kwa maana nyingine Bunge linakumbukumbu zote na kutokana na kuwa na kumbukumbu ni rahisi zaidi kutoa elimu kwa jamii ya Wafugaji,wakulima pamoja na Wavuvi ili kuweza kuboresha shughuli zao za kila siku”alieleza Patson.
Kwa upande wake Zuhura Mtatifikolo,kitengo cha habari za Bunge alisema maonesho ya nanenane ni chachu ya maendeleo kwa wakulima,wafugaji pamoja na wavuvi kwa kupata elimu ya sekta hizo.
“Maonesho haya ni kwa ajili ya kuwapatia watu wa kada hizo elimu ya uendeshaji wa Shughuli mbalimbali za uzarishabi bora na si bora uzalishaji.

“Kama kila mmoja atapata elimu ya kutosha juu sekta husika ambayo yupo mfano mkulima,mfugaji na Mvuvi wataweza kufanya kazi zao kwa tija na kujiongezea kipato kikubwa na kuliongezea taifa pato badala ya kufanya kazi kwa mazoea”alieleza Zuhura.
Naye Waziri wa Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dk.Tzeba alisema ni jambo jema kwa kila mwenye ujuzi na nafasi ya kujua jambo akatoa elimu kwa sekta hizo muhimu.
Alisema nchi ikiwa na mkakati wa kuelekea katika uchumi wa kati na wa Viwanda ni lazima wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi wakapatiwa elimu ya kutosha juu ya ufanyaji wa kazi zao badala ya kufanya kazi kwa mazoa na bila kuwa na tija.
“Sekta ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi ni kati ya sekta ambazo zinatakiwa kupewa kipaumbele kwa lengo la kuwa na uzalishaji bora na wenye tija ili kulifikisha taifa katika uchumi wa kati na uchumi wa Viwanda” alisema Dk.Tzeba.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG