BANDA MEDIA BLOG

RAIS Magufuli: Baadhi ya Mawaziri KATIKA Serikali Yangu ni Wapumbavu


Mh.Rais akiwa Tanga mchana wa leo aliwaambia wananchi kwamba baadhi ya mawaziri katika Serikali yake ni Wapumbavu.

Alitoa mfano wa Profesa Muhongo aliyemwagiza kuhakikisha flow meter kwa ajili ya kupima viwango vya mafuta yanayoteremshwa bandarini lakini hakufanya hivyo mpaka alipomtumbua.

Hapo awali asubuhi ya leo alimwambia Charles Mwijage kuwa anamkwaza kwa kutochukua hatua za kuwanya ng'anya viwanda walioshindwa kuviendeleza. Ninaungana na Mh. Rais 100% katika kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa.

Swali langu: Je, lugha na kauli za Mh. Magufuli zinaweza kuwa na madhara gani katika Serikali anayoiongoza? Hasa kwa wasaidizi wake wakiwemo Mawaziri?

  Chanzo:Jamii Forums/lancanshire

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG