| Waziri
wa Nchi OR TAMISEMI Mhe. George B. Simbachawene akitoka kukagua jengo la
madarasa mawili shule ya sekondari Loiborsiret wilayani Simanjiro mkoani
Manyara alipofanya ziara mkoani humo jana |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) amepokea maoni ya wananchi wa vijiji vya Sukuro
na Kityangale kwa ajili ya kutoa suluhu ya mgogoro wa kitongoji cha Katikati
kinachogombewa na pande hizo mbili tangu mwaka 2009.
Akitoa maelezo ya awali Mhe. Simbachawene amesema
uamuzi wa Serikali utazingatia maslai ya wananchi na nchi kwa ujumla na sio
maslai binafsi kama ambavyo makundi makundi yalivyo katika mgogogoro huo wa
muda mrefu ambao hauna tija kwa wananchi na maendeleo yao.
“Mimi nimeona na ninachukua maoni yenu bila hata ya
kupiga kura, na sitaki kusema nani ameshinda, sawa jamani, acha niende,
nitafakari, na nitarudisha majibu ndani ya siku kumi na nne na majibu hayo
yatakuwa ndiyo ya mwisho”
Amesema serikali haiwezi kubaki kimya na haiamui,
lakini uamuzi wa suala hili utazingatia sana maslai mapana ya wananchi,
shughuli za wananchi na Taifa kwa ujumla
wala hautaunga mkono kikundi fulani cha watu.
Aidha, alisema uamuzi wa kitongoji cha katikati
utazingatia zaidi kuwepo kwa amani na usalama wa eneo lenyewe ili waweze
kufanya shughuli za maendeleo na wao wenyewe kwa ujumla.
“Jambo hili ni lazima liishe na litaisha mapema sana,
nitakuja kulisema hapa na ndio utakuwa uamuzi wa Serikali. kwa hiyo, mimi
nimepokea, uamuzi utakuja ndani ya siku kumi na nne wenye maslai ya watu na
maslai ya nchi kwa ujumla”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel
Bendera amesema ugawaji wa mipaka mipya ya maeneo hayo itazingatia amani na
utulivu kwani historia huko nyuma inaonyesha kuwa kulikuwa na ugomvi ambao
hauishi na kuwataka wananchi kusubiri uamuzi wa mwisho wa Serikali.
Mgogoro wa kugombewa kitongoji cha katikati ni wa muda
mrefu kwani hata mipaka yake haijawekwa wazi kwa kuwa mazingira ya Maafisa
Ardhi kwenda kupima yamekuwa magumu na wameshindwa kwa kuwa jamii hiyo kijiji
cha Sukuro, Kityangale na kitongoji cha katikati inayoishi hapo haitoi
ushirikiano wa kuonyesha mipaka halisi ya kitongoji hicho ili kila mmoja abaki
na eneo kubwa ijapokuwa kitongoji kina eneo kubwa la kutosha kuwa kijiji.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI
Mhe. George Simbachawene ametembelea shule za sekondari wilayani Simanjiro Loiborsiret
na kujionea ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na maabara ambao umefanikiwa
kwa kiwango kikubwa na mwisho alitembelea shule ya sekondari Emboreet yenye
kidato cha tano na kuahidi kuwaongezea idadi ya wanafunzi ndani ya muda mfupi.
Pia akiwa shuleni Emboreet ameongea na wazazi, walimu na wanafunzi na kuwapongeza
kwa kazi nzuri wanayoifanya iwepo ya marafiki wa Shirika la ECLAT Foundation ya
Tanzania na Upendo society ya Ujerumani, wakiwemo Foundation for Care and
education ya Germany waliotoa fedha za kujenga majengo mbalimbali ya shule hiyo
kama shumba za wal;imu na maabara.
Waziri Simbachawene amehitimisha ziara wilayani
Simanjiro mkoani Manyara kwa kuiagiza mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na
Taasisi za Serikali kuendelea kupanda miti na kutunza mazingira kwa maslai ya
wananchi na Taifa kwa ujumla.
Tags
SIMBACHAWENE