Timu ya Ruvu Shooting ya mkoani
Pwani imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida United mchezo
wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Mabatini ukiwa ni mchezo wa
maandalizi ya msimu mpya unaotarajia kuanza Agosti 26.
Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao
likifungwa na Full Maganga dakika ya 20 hata hivyo goli hilo halikudumu
kwani dakika ya 26 mshambuliaji wa zamani wa Jkt Ruvu Atupele Green
aliweza kuisawazishia Singida hadi mapumziko timu hizo zilikwenda zikiwa
zimefungana 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote kufanya mabadiliko hata hivyo hakuna timu ambayo iliweza kupata
goli hadi dakika 90 kipyenga kinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu
sawa kwa kufungana goli 1-1.
Singida United wanatarajia kesho
kuwasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo mwingine wa kirafiki
dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga mchezo ambao utapigwa
siku ya Jumamosi na unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini
kuona kocha wa zamani wa Yanga,Hans Van Der Pluijm anakutana na timu
yake ya zamani ambayo ipo chini ya George Lwandamina.
Tags
SINGIDA UNITED