Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania bara timu ya Yanga imeishushia kipigo cha mbwa mwitu cha magoli
5-0 timu ya Vijana chini ya miaka 20,Moro Kids katika mchezo wa kwanza
wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Seminar asubuhi Leo huko mkoani
Morogoro.
Mshambuliaji raia wa Zimbabwe
Donald Ngoma ambaye msimu uliopita hakucheza msimu mzima kutokana kuwa
na majeruhi ameendeleza wimbi la kufumania nyavu mara baada ya kufunga
magoli mawili na kuendelea kuonekana kuwa ni tegemeo katika kikosi cha
kwanza cha Kocha George Lwandamina.
Kiungo mshambuliaji Mpya kutoka
Mbeya City Raphael Daudi ameanza kwa kufunga bao moja katika ushindi huo
magoli mengine yakifungwa na Amissi Tambwe na kinda Yussuf Mhilu kila
mmoja akifunga goli moja.
Kikosi cha Yanga kimepiga kambi
Morogoro ambapo wamefikia katika Hoteli ya B-Z eneo la Nane Nane huku
wachezaji wote walipewa nafasi ya kucheza na kocha Mkuu na kikosi hicho
kinatarajia kurejea kesho jijini Dar es salaam ambapo Jumamosi Agosti 5
watashuka uwanjani kucheza na Singida United kwenye uwanja wa Taifa na
mchezo wa pili watacheza Agosti 12 na timu ambayo itatangazwa baadaye.
Tags
yanga