KATIKA Maonyesho ya Nanenane kanda ya kati Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama pori (TAWA) limeonekana kuwa kivutio kwa wananchi wa mikoa ya Dodoma na Singida.

Hali hiyo imetokana na kuwepo vivutio vingi vya wanyama hai pori ambao wameletwa huku wanyama wengine wakiwa ni mara ya kwanza kupelekwa katika maonyesho hayo tangu yaanze kuoneshwa mkoani hapa.
Wananchi mbalimbali wamesema kuwa katika maonesho ya nanenane kanda ya kati kivutio kikubwa ni wanyama hai pori kwani kwa sehemu watanzania wanejikuta wakifanya utalii wa ndani.
Mmoja wa wananchi Devison Mutatina, amesema licha ya kuwa katika mabanda ya TAWA kuna msongamano mkubwa lakini wananchi wamefaidi kwa kuwaona wanyama live.
“Tumezoea kuona wanyama kupitia runinga lakini hapa unatoa sh.book (1000) unafaidi kuona wanyama mbalimbali hapa kuna Tausi,nyati,makobe wakubwa, Mamba,Tusi ambao wanaonekana zaidi Ikulu, Nyati, Ndege aina aina ya taji Korongo.
“Pia tumeweza kushuhudia Simba dume na jike huku tukipata maelezo ya kina kuwa simba uweza kula nyama kilo 40 kwa siku na baada ya kushiba anaweza kuishi siku tatu bila kula hizo zote ni faida za Nanenane kupitia banda la TAWA”alisema Mutatina.
Naye Afisa habari na Mahusiano wa Mamlaka hiyo Twaha Twaibu, alisema kwa sasa Mamlaka hiyo imeboresha mazingira ya Maonesho ya Nane nane sambamba na kujikita katika utoaji elimu kwa wananchi.
Amesema maonyesho yameendana na utoaji wa elimu kwa jamii na kuwaeleza faida ya kufaya utalii wa ndani sambamba na utunzaji wa mazingira na kuwalinda wanyamapori hai bila kuwadhuru.