Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akiwasalimia wananchi katika Uwanja wa Nsololo jimbo la Igalula Wilaya
ya Uyui mara baada yakuwasili leo August 12.2017 na kufanya mkutano wa
hadhara katika Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM Taifa na Mkuu wa
Wilaya Mstaafu Bwana Jackson Masome .walipo kutana katika mkutano wa
hadhara leo August 12.2017 katika Wiaya ya Uyui Tabora Waziri yupo Mkoa
wa Tabora kwa ziara ya Kikazi
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa na Mkewe Mama Majaliwa wakiwasalimia wananchi katika
Uwanja wa Nsololo jimbo la Igalula Wilaya ya Uyui mara baada yakuwasili
leo August 12.2017 na Waziri Mkuu kufanya mkutano wa hadhara katika
Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora
………………………………………………………………………..
*Ataka waache kutoa hovyo vibali vya uvunaji misitu
*Ahimiza utunzaji misitu, mazingira
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekemea tabia ya kutoa vibali vya uvunaji mbao inayofanywa na maafisa
misitu wa TFS ambao wako chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Ametoa onyo hilo leo mchana
(Jumamosi, Agosti 12, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwenye mkutano uliofanyika kata ya Goweko,
wilayani Uyui mkoani Tabora.
Waziri Mkuu alifikia hatua hiyo
baada ya kumhoji Afisa Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) Bw. Juma Kazimoto na Afisa Misitu wa Wilaya, Bw. Jared Nzilorera
na kubaini kuwa hawafanyi kazi kwa kushirikiana.
“Hapa kuna uvunaji mkubwa wa misitu. Je kuna mtu anafuatilia kama wanavuna kwa usahihi?” alihoji Waziri Mkuu.
Akijibu swali la Waziri Mkuu,
Bw. Kazimoto alisema Uyui hakuna uvunaji lakini wanaovuna wanatoka
Sikonge na kuja kuuza mbao Uyui.
Alipoulizwa Afisa Misitu wa
Wilaya, ni kwa kiasi gani wanapeana taarifa na mwenzake wa TFS ambao
wanaletwa na wizara, alitoa majibu ya kujichanganya hali iliyomfanya
Waziri Mkuu aamue kukemea tabia yao ya kutoa vibali bila kuwahusisha
wenzao wa Halmashauri.
“TFS mmejiingiza kwenye kuvuna
misitu, na mnawaover-power DFOs (wale wa Halmashauri). Hawa walioko
kwenye Halmashauri ndiyo wanaolinda misitu yote ambayo iko ndani ya
wilaya husika.”
“Tatizo hili liko nchi nzima, ni
la ushindani kati ya maafisa misitu wa TFS na wale wa Halmashauri.
Misitu yetu inakwisha sababu mnaimaliza nyie kwa kutoa vibali bila
kuwashirikisha wenzenu.
Alimwagiza Kaimu Mkuu wa Wilaya
ya Uyui, Bi. Queen Mlozi asimamie suala hilo. “DC wewe ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, simamia jambo hili na usisitize
utunzaji wa mazingira na upandaji miti,” alisema.
Alisema ukataji miti ovyo
umechangia kukauka kwa vyanzo vingi vya maji. “Mhandisi wa Maji
anahangaika kuchimba visima lakini hakuti maji sababu miti imekatwa ovyo
na ardhi tepetevu imekauka. Watumishi wote nendeni vijijini
mkahamasishe utunzaji wa mazingira,” alisema.
Kwa mujibu wa hali ilivyo
sasa, kila mkoa una Afisa Misitu wa Mkoa, kila wilaya imeajiri Afisa
Misitu wa Halmashauri, lakini Wizara pia imeajiri Maafisa wa
Misitu kutoka TFS katika ngazi za mkoa na wilaya.
Tags
MAJALIWA