Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa wazazi
wenye tamaa ya fedha ambao wamekuwa wakiwakatisha masomo mabinti zao kwa
ajili ya kuwaozesha.
Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana Wilayani Uyui katika mkutano wa hadhara
Alisema kuwa kuanzia sasa
Watendaji wanatakiwa kuwakata na kuwafikisha katika vyombo vya dola bila
woga wazazi wa binti na wale wa kijana wanakatisha masomo ya watoto wa
kike kwa lengo la kuwaozesha.
Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali
haitawavulia wazazi na watu wanaochangia kurudisha maendeleo ya
wasichana kisingizio cha kuwafungisha ndoa wakati bado ni wanafunzi.
“Nawaagiza Watendaji wote
kuwakata wazazi wa binti na wale kijana ambao mtawakuta wakiwa
wanawaozesha mabinti wao ambao kimsingi walipaswa kuwa shule……msimuogope
mtu wakamateni wote wawe wazazi wa binti hata wa yule anayetarajia kuoa
ili hatua kali za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa” alisisitiza
Mhe. Majaliwa.
Aliwaonya pia vijana ambao
wanamiliki na kuendesha pikipiki maarufu kama boda boda ambao wamekuwa
wakiwapakia wanafunzi kwa lengo la kuwarubuni ili wajihusishe na vitendo
vya ngono kuacha mara moja.
Waziri Mkuu alisema mtu atakayekamatwa Serikali itamfikisha Mahakamani ili aweze kupata adhabu kali.
Alisisitiza kuwa ni vema wakaacha wanafunzi hao wakasoma na sio kuwarubuni.
Mkoa wa Tabora ni miongoni mwa mikoa mitatu hapa nchini inayoongoza kwa mimba na ndoa za utotoni.
Tags
UKATILI