Mbunge wa kigoma Ujiji na Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi kabwe
ameilaani kauli ya Kaimu Msemaji mkuu wa Serekali Zamaradi kawawa kuwa
wanasiasa ndio Wanashirikiana na kampuni za njee kuhujumu nchi "Hakuna
mwanasiasa anayeweza kushirikiana na kampuni za kigeni kuhujumu nchi.
Mimi binafsi filosofia yangu ni rahisi Sana ' My Country, Right or Wrong
'. Maneno yanayosambazwa kuwa nimeshiriki kuwezesha Ndege ya Bombardier
iliyonunuliwa na Serikali Kwa niaba ya ATCL kukamatwa huko Canada ni takataka tu zinazosambazwa na wapika propaganda."

Akisema kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto ameitahadharisha serekali kuwa swala la Ndege kuzuiwa lisifanywe kishabiki kama ulivyo ushabiki wa mpira "Suala la Ndege yetu kuzuiwa Canada lisifanywe Ni suala la ushabiki Kama ushabiki wa mpira. Ni suala la Nchi hili na mjadala wake uwe na hadhi hiyo.
Kitendo cha Msemaji wa Serikali kulaumu wanasiasa Kwa jambo la kisheria Kama hili ni utoto." Alisema Zitto
"Serikali lazima ifahamu kuwa ni lazima ihojiwe na iwe tayari kutoa majibu. Sisi kama vyama vilivyo Nje ya Serikali Ni wajibu wetu kuhoji jambo lolote. Pia ni haki yetu kupata Taarifa zozote kutoka mahala popote zitakazosaidia kuisimamia Serikali. Wajibu wa Serikali ni kujibu hoja zinazoibuliwa. Majibu ya Msemaji wa Serikali yanataka kuligeuza suala hili kuwa la kisiasa na watu wameangukia kwenye ushabiki huo. Hili ni suala la kisheria na suala la nchi ambayo sisi wote tuna maslahi ya kuona inakwenda mbele" Nchi kudaiwa sio dhambi. Hata mataifa makubwa duniani yanadaiwa. Watu binafsi tunadaiwa sembuse Serikali? Mimi ninadaiwa madeni ya uchaguzi mpaka Sasa na wengine wamenipeleka mahakamani. Sio dhambi kudaiwa. Muhimu ni 1) Deni limetokana na Nini? Ni maamuzi mabovu ya kisiasa? 2) unalipa deni hilo au kuweka mikakati ya kulipa? Aliongea Zitto
Hii ni nchi yetu sote. Hakuna mwenye hatimiliki ya ukweli. Ukweli pia haupendi kupindwa pindwa. Serikali itoke kueleza nini kimetokea mpaka Ndege kuzuiwa, iachane na tabia ya hovyo ya kutafuta mchawi ' kwamba eti wanasiasa Ndio wamesababisha '. Kutafuta mchawi ni kutowajibika Kwa maamuzi ya Serikali yenyewe. alimalizia Zitto

Tags
ZITO KABWE