Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua majengo yaliyo karabatiwa na serikali katika sekondari ya mpwapwa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua jiko la kisasa linalo jengwa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wa Mpwapwa sekondari.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Kamati ya ujenzi wa Mpwapwa sekondari.
Baadhi ya madarasa ya Mpwapwa sekondari yaliyo karabatiwa.
……………………………………………………………………………..
VIONGOZI wa Wilaya ya Mpwapwa
mkoani Dodoma wameishukuru serikali kwa kukarabati sekondari ya Mpwapwa
ambayo majengo yake yalikuwa yana hali mbaya.
Viongozi hao wametoa shukrani
hiyo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo
alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua ukarabati wa shule hiyo.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule
88 kongwe zinazokarabatiwa na serikali ambapo katika awamu ya kwanza
ukarabati umeanza kwa shule 43.
Katika shule hiyo, Serikali
imefanikiwa kujenga bweni moja jipya la wasichana, ukarabati wa mabweni
12 ya wavulana, ukarabati wa vyumba vya madarasa 22, bwalo la chakuka
pamoja na jiko, maktaba, maabara tatu, ofisi za walimu, mfumo wa maji na
umeme ambapo jumla ya sh.bilioni 1.2 zimetumika.
Akizungumza na viongozi katika
ziara yake,Naibu Waziri Jafo ameipongeza Kamati ya ujenzi kwa
kufanyakazi bila kuchoka na kufanikisha kuibadili kabisa shule hiyo
ambayo kwasasa imegeuka kuwa shule bora ya kisasa tofauti na ilivyokuwa
awali.
Naibu Waziri Jafo amewataka
wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii kwani serikali ya Dk. John
Magufuli imeamua kuboresha miundombinu pamoja na vifaa vya kutolea elimu
kwa lengo la kufanikisha elimu bora hapa nchini.
Tags
MPWAPWA