Na: Thobias Robert.
Katika kutimiza ndoto ya Tanzania ya
uchumi wa kati unaotegemea uzalishaji viwandani, wadau mbalimbali wa
maendeleo wamezidi kujitokeza na kutoa mawazo yatakayosaidia kukuza
sekta za kiuchumi ili kutimiza ndoto hiyo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza katika Dkt. Samson Kibona,
kutoka Antipa Herbal Clinic amesema kuwa uchumi wa viwanda utaokoa
kilimo cha Tanzania na kupandishwa thamani ya mazao yalimwayo hapa
nchini na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa.
Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam
katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa lengo la kuelezea
mbinu za kilimo cha kisasa, kutoa ombi kwa serikali juu ya kusimamia
kilimo hicho chenye tija na kitakachopunguza uagizwaji wa bidhaa
zitokanazo na kilimo kutoka nje ya nchi.
“Tanzania ya viwanda itaokoa sekta ya
kilimo, kupandisha thamani ya mazao na kufanya mazao yanayolimwa nchini
kutosafirishwa nje badala yake bidhaa zitokanazo na mazao hayo kama vile
mafuta ya kupikia, vyakula vya kawaida, kama biskuti, nafaka halisi ya
unga ndizo zitasafirishwa au kuuzwa nje na kuongeza fedha za kigeni,”
alieleza Dkt. Kibona.
Aidha Dkt. Kibona ambaye pia ni mkulima wa
kati wilayani Momba alisema kuwa, serikali haina budi kutumia mfumo wa
kilimo cha umwagiliaji (Canal System) kama ambavyo mataifa ya Israel,
Pakstani na India yamekuwa yanatumia njia hiyo, lakini pia kuondoa
utegemezi wa kilimo cha mvua pekee yake ambacho kimekuwa kikitumiwa
kutoka karne hadi karne hapa nchi ambacho kimekuwa kikiligharimu taifa
pindi hali ya hewa inapobadilika.
Vilevile serikali haina budi kutumia mbegu
za kisasa zinazozalisha mazao ya kutosha na yenye tija kwa taifa na
kipato cha mtu mmoja mmoja kuliko kuendelea kutumia mbegu za zamani
ambazo zimekuwa zinaathiriwa na kushambuliwa na maradhi pamoja na
wadudu.
Aliendelea kusema kuwa kwa taifa la
Uingereza lina asilimia 20 ya watu wanaojihusisha na kilimo linatumia
mbinu ya Green house ambayo ni njia ya kuchimba shimo na kutumia mitambo
ya kumwagilia shamba (Pivot injection system) lakini nchi ya Tanzania
ina wakulima wanaofikia zaidi ya asilimia 75 lakini bado wanatumia njia
za asili katika uzalishaji wao.
“Tanzania imekuwa ikipokea bidhaa
mbalimbali kutoka nje ya nchi kama vile mitumba, viatu pamoja na bidhaa
zingine, ifike hatua tuanze kutoa bidhaa Tanzania tupeleke nje ya nchi
ili turudi na dola mikononi ili tuijenge nchi yetu kwa kutumia pesa zao
na siyo wao pekee kutuletea bidhaa zao hapa nchini,” aliezea Dkt.
Kibona.
Aidha aliongeza kuwa kwa sasa soko la
mazao ya mboga mboga zinazozalishwa hapa nchini ambalo limekuwa na soko
kubwa nje ya nchi, serikali haina budi kuhakikisha kuwa inaongeza
msukumo na utoaji wa mbolea kwa wakulima ili kurahisisha uzalishaji wa
mbogamboga hizo. Vilevile mazao ya mahindi, maharage, soya yanapaswa
yageuzwe kuwa mazao ya biashara yanaoyotegemewa kwa pato la taifa kuleta
pesa za kigeni kwani mazao hayo yanaishia hapa nchini pekee.
Dkt. Kibona alimuomba Rais Dkt. John
Magufuli ahakikishe kuwa kuna upatikanaji wa kutosha wa huduma za
ulinzi, umeme, benki, afya pamoja na maji hususani maeneo ya vijijini
ili wakulima waweze kuzalisha mazao ya biashara yenye tija kwa ajili ya
ushindani wa kimataifa.
“Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, iwe
inatoa motisha kwa wakulima kama vile kuwapa tuzo wakulima wanaozalisha
na kuuza mazao mengi ya biashara na kulipatia taifa fedha za kigeni,
kutoa punguzo la bei za pembejeo kwa wakulima hasa vijijini, pamoja na
kusimamia vyema bei za mazao ya kilimo hapa nchini na nje ya nchi kwa
wakulima wetu,” alifafanua.
Dkt. Kibona ni mtaalamu wa masuala ya
kilimo ambaye pia anamiliki kampuni yake inayojihusisha na kilimo
wilayani Momba mkoani Songwe ambaye amekuwa akitumia kilimo chake kama
shamba darasa kwa Wananchi na viongozi wa wilaya na Mikoa ya jirani.
Vilevile kwa sasa ana mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata mpunga
katika eneo la kijiji cha Luasho.
Dkt. Kibona: Tanzania ya Viwanda Itaokoa Kilimo Hapa Nchini

Tags
VIWANDA