Rais Magufuli akihutubia.
RAIS John Magufuli ambaye leo
Oktoba 14, 2017 ni Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo
cha Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Kilele
cha Mbio za Mwenge amesema amejisikia faraja kuwa mgeni rasmi kwenye
maadhimisho hayo ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki maadhimisho hayo
tangu awe Rais.
Aidha, Magufuli amemuelezea Hayati
Mwl. Nyerere kama kiongozi shupavu alipeginani maslahi ya wanyonge na
kupambana na wakoloni katyika kufanikisha kupatikana kwa Uhuru wa
Tanganyika, Zanzibar na nchi nyingine za Afrika.
Amesema Nyerere alianza harakati
za siasa mwaka 1953 baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha TAA
ambacho baadaye kilizaa TANU huku akiwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari
ambayo kwa sasa inaitwa Pugu Sekondari ambapo baadaye aliacha kazi hiyo
ya kiufundisha na kujikita kwenye siasa za ukombozi.
Magufuli piua amesema iwapo Mwl.
Nyerere angekuwa kiongozi mwenye tamaa au mbinafs, basi angechukua fukwe
zote za Msasani, jijini Dar es Salaam na kuzifanya ziwe za mali yake,
lakini hakufanya hivyo kwa sababu ya uzalendo mkiubwa aliokuwa nao.
Rais amesisitiza kuwa kamwe
hatokukubali mbio za Mwenge wa Uhuru zifutwe katika kipindi chake cha
uongozi, kwani mwenge huo una manufaa makubwa kwa Taifa ikiwemo kuzindua
miradi mbalimbali za maendelo pamoja na kuwa nembo muhimu kwa Taifa
letu.
Amesema wanaotaka mwenge huo
ufutwe huenda hawajui historia ya nchi hii na kwamba kama wanaweza
kukubali fimbo na kombe la dunia vikaletwa nchini na wakavipokea basi
mbio za mwenge ni muhimu zaidi kuliko wanavyodhani.
Akizungumzia hali ya uchumi wa
nchi, rais amekanusha wanaodai kuwa uchumi umeshuka huku akieleza kuwa
uchumi wa Tanzania unazidi kupanda hukui mfumuko wa bei ukishuka na
matokeo yake yanaonekana kwenye bidhaa pamoja na kushuka bei zake. Pia
ameeleza kuongezeka kwa viwanda na wawekezaji wa kibiashara hapa nchini.
Tags
Mbio za Mwenge
