BANDA MEDIA BLOG

HALI YA TAHARUKI YATANDA KWA WANANCHI BAADA YA KUKUTA MZOGA WA KUKU UMEVISHWA SANDA HUKU UKIWA NA MADAWA YA KIASILI


Mzoga wa kuku ambaye amefungwa na sanda kwa maelezo ya wananchi ambao walikuwa Nje ya Nyumba ya Bw Emmanuel Kabodi ambapo ndipo tukio hilo limetokea linalo husishwa  na imani za kishirikina.

Mama Mwenye Nyumba ambapo tukio hilo limetokea Bi,Scolastica Nicodemo  akizungumza na moja kati ya viongozi wa dini wakati alipofika kwenye familia hiyo kuona tukio hilo la kusitajabisha.

Baadhi ya wananchi wakishangaa jambo ambalo limetokea katika mtaa wa 14 kambarage.

Viongozi wa dini wakiteketeza vitu pamoja na mzoga huo ambao umekutwa kwenye Nyumba hiyo.

Baadhi ya watu wakishangaa tukio hilo la kusitajabisha.    
PICHA NA JOEL MADUKA 
/

Katika hali
isiyo ya kawaida wananchi wa Mtaa wa 14 Kambarage Kata ya Buhalahala Wilaya na
Mkoa wa Geita wamejikuta wakipigwa na Butwaa
baada ya kukuta mzoga  wa kuku  ukiwa
umevishwa sanda  kwenye familia ya
Emmanuel  Kabodi.
Mama wa
familia hiyo Bi Scolastica Nicodemo ameelezea kuwa   wakati
akifanya usafi  aliona  nyuma
ya geti  kuna kitu kimefungwa na
shuka  jeupe na alipojaribu  kukiangalia aligundua  ni sanda imefungwa kuku na ndipo walipofanya
maamuzi ya kumwita mchungaji kuja kujionea.
Askofu wa
kanisa la  TMRC Mkoani Geita Stephano
Saguda  ameihasa jamii kuachana na
maswala  yanasosadikiwa kuwa ni ya
kishirikina  kwani vitendo hivyo
havimpendezi Mungu na havikubaliki kwenye jamii ya watanzania .
Mjumbe wa
Mtaa Huo Stephano Mayovu Matata,amesema
tukio hilo ni mara ya pili kwani mara ya kwanza lilitokea tukio la
kufukuliwa  kwa mtoto  na kwamba ni vyema kwa mtu ambaye anafanya
vitendo hivyo kuachana  navyo mara
moja  kwani wakimbaini mtu wa namna hiyo
hawataweza kumvumilia.
Wananchi
ambao walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo wamesikitishwa na kitendo hicho
kutokana na matukio hayo kuendelea kujitokeza mara kwa mara.
Mtaa  wa 14 Kambarage umeendelea kukumbwa na
vitendo vinavyosadikiwa ni vya Imani za kishirikiana vya mara kwa mara na  kusababisha
hofu kubwa kwa watu ambao wanaishi maeneo hayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG