Mhasibu
wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph, Elizabeth Asenga (40)
amehukumiwa kulipa faini ya Sh 5 milioni ama kutumikia kifungo cha mwaka
mmoja jela baada ya kukutwa na hatia katika shitaka la kutuma ujumbe wa
kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya
Kisutu, Huruma Shaidi, ametoa hukumu hiyo leo Jumanne baada ya kupitia
ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na utetezi
uliotolewa na mshtakiwa mwenyewe na kumhukumu mshtakiwa huyo kulipa
faini ya Sh 5 milioni ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kukwepa adhabu ya kifungo.
Kesi hiyo namba 317 ya 2016
mshtakiwa huyo alidaiwa kuwa Agosti 6, 2016, aliwasilisha ujumbe wenye
mazingira ya kumkashifu Rais Magufuli kwa njia ya WhatsApp kwenye kundi
la kijamii liitwalo STJ Staff Social Group.
Mshtakiwa huyo aliandika ujumbe
usemao: ‘Godmorning humu. hakuna Rais kilaza kama huyu wetu duniani,
angalia anavyompa Lissu umashuhuri, fala lile, picha yake ukiiweka
ofisini ni nuksi tupu. Ukiamka asubuhi, ukikutana na picha yake ya
kwanza siku inakuwa mkosi mwanzo mwisho.”
Baada ya kusomewa shitaka hilo
alikana na alikuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili ambao
kila mmoja wao alisaini hati ya dhamana ya maneno ya Sh 2 milioni.
Tags
JELA
