Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
akizungumza na washikriki wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya
maadili na haki za binadamu kitaifa katika ukumbi wa mikutano Hazina
Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
akizungumza na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati
wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu
kitaifa Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
akizindua rasmi maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za binadamu
kitaifa katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma, leo
Baadhi ya washiriki waliohudhuria
katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu
kitaifa katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
akimkabidhi kitabu cha muongozo wa maadili na haki za binadamu
Katibu Mtendaji Tume ya haki za binadamu na Utawala Bi. Mary Massay
katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma,leo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
pamoja na baadhi ya viongozi kutoka katika taasisi mbalimbali za haki
za binadamu na mwanafunzi wakionesha kitabu cha muongozo wa Maadili
na haki za binadamu wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho mjini Dodoma.
…………….
Nteghenjws Hosseah,OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanasimamia uzishwaji
wa klabu za maadili katika shule zote za Msingi zilizopo katika maeneo
yao.
Waziri Jafo pia amewataka Maafisa
Elimu Msingi na Sekondari Nchini kutekeleza agizao hilo na
kuwasilisha ripoti juu ya klabu ngapi za maadili zimeanzishwa katika
maeneo ambayo wanayasimamia na taarifa iwasilishwe kabla ya wake April
30,2018.
“ Ifikapo Tar. 30 mwezi wa nne
mwakani kila afisa elimu ahakikishe anandaa ripoti ya Utekelezaji
inayoonyesha katika Shule kadhaa klabu ngapi za maadili zimeundwa na
hayo ni miongoni mwa mambo nitakayoyafanyia tathimni “
Waziri Jafo alitoa maagizo hayo
mapema leo wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Maadili Kitaifa
ambayo imekwenda sambamba na uzinduzi wa klabu kumi na tano za maadili
uliambatana na uzinduzi wa mwongozo wa klabu hiyo uliofanyika katika
ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.
Aliongeza kwa kuwataka maafisa
elimu wote wahakikishe waanzisha klabu hizi, kuzilea na na kuziwezesha
kwakuwa zoezi hili likifanywa kwa umakini na kwa ukubwa wake
litaweka msingi imara katika kupata viongozi wenye uweledi na
kusaidia kutengeneza vijana imara walioiva kimaadili na kuondoa
changamoto ya kukosekana kwa maadili katika jamii inayopelekea uvutaji
na utumiaji wa madawa ya kulevya, mimba na na ubadhilifu.
Wakati wa uzinduzi huo Waziri Jafo
amewataka Viongozi na wananchi wote kuweka uzalendo mbele na uadilifu
katika kutekeleza majukumu yetu yatakayoenda sambamba na kulinda
rasilimali za Taifa hili.
“Bila uzalendo tutapoteza muelekeo
katika Nchi yetu na rasilimali zote za Taifa hili zitapotea kwa
kutumiwa na watu wachache na zaidi ya hapo vizazi vijavyo vitakosa
kunufaika na rasilimali hizi ambazo ni muhimu kwa ustawi wao na ni haki
yao ya msingi” alisema Waziri Jafo.
Katika uzinduzi huo Mhe. Jafo
amezitaka Taasisi zote zinazoshughulikia maadili kufanya kazi kwa
uadilifu kwa kutekeleza Mkakati dhidi ya Rushwa na Mpango wa
Utekelezaji wa Awamu ya Tatu uliozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan ili kuendeleza ajenda ya uzalendo na kuwafundisha
wananchi kuwa wazalendo katika jamii.
Aidha amezishukuru ofisi
mbalimbali zinazoratibu haki za binadamu kwa kazi nzuri wanazozifanya
na kutoa rai kwa wadau wengine hasa Watendaji wake Wakuu
kujitafakari na kuona ni jinsi gani wanaweza kushiriki katika kupambana
na rushwa na kutoa elimu ya Uadilifu katika utoaji wa huduma kwa
wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Harold Nsekela alisema Siku ya maadili
inatokana na Siku ya Kimataifa ya kuzuia na kupambana na rushwa na
maadimisho ya siku ya haki za Binadamu na kilele cha Siku hii
ktafanyika Dec 10 na kwa kauli mbiu ya inayobeba maadimisho haya ni “Uwajibika, piga vita rushwa zingatia maadili ,haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumi wa kati”
Naye Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad amesema kuwa kupitia mada
zitakazowasilishwa katika uzinduzi huo zitawapa washiriki maarifa ya
kuendelea kufanya kazi kwa uweledi na kuongeza ubunifu ili kuleta tija
na maboresho katika utendaji.
Tangu maadhimisho ya Siku ya
Maadili kuanza yamesaidia kuongeza chachu na kuamsha ari kwa wananchi
kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika katika kulinda
haki za Binadamu, kupiga vita rushwa na Ufisadi, uzembe na ubadhirifu
wa mali za Umma.
Tags
MAADILI