kwa uwamuzi huo sasa Rais Kenyatta anatarajiwa kuapishwa Jumanne ya wiki ijayo.
Jaji Mkuu David Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.
Kesi ya zilifunguliwa na wananchi wawili ambao ni mbunge wa zamani Bw Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif zimetupiliwa mbali.
"Uchaguzi wa 26 Oktoba umedumishwa, sawa na ushindi wa Bw Kenyatta. Kila upande utasimamia gharama yake," amesema.
Uamuzi wa kina utatolewa katika kipindi cha siku 21.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais wa marudio akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.
Kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.
Tags
UCHAGUZI KENYA