Kufuatia hatua iliyochukuliwa mwezi Aprili mwaka huu ya kuufunga msikiti maarufu wa Clichy, Waislamu wa eneo hilo wamekuwa wakisali Sala ya Ijumaa barabarani kulalamikia uamuzi huo.
Waislamu nchini Ufaransa wanasema serikali haijawapatia eneo mwafaka la ardhi kwa ajili ya kujenga msikiti mpya na kwamba licha ya kukubaliana na udharura wa suala hilo hadi sasa haijachukua hatua yoyote kuhusiana na jambo hilo.
Jumuiya moja ya Waislamu ya mjini Paris imetangaza kuwa Sala ijayo ya Ijumaa itasaliwa katikakati ya mji mkuu huo wa Ufaransa.
Kuenezwa hisia za chuki na hofu dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika nchi za Magharibi kumewafanya Waislamu wa nchi hizo wakabiliwe na mbinyo na mashinikizo makubwa katika kutumia haki yao ya uhuru wa kuabudu.../
Tags
UFARANSA