Dr. Qasim Sufi Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji akifanyiwa majaribio katika mfumo wa
utambuzi wa sura (Facial Recognition and matching system) katika Uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Kamishna wa Uhamiaji (Usimamizi
na Udhibiti wa Mipaka) Samwl Magweiga (wa kwanza kulia) akisikiliza kwa
makini namna mfumo huo unavyofanya kazi wakati wa ufungaji wa vifaa
vyenye mfumo huo.
Kamishna wa Uhamiaji (Usimamizi
na Udhibiti wa Mipaka) akikabidhiwa nyaraka za mfumo huo na Mwakilishi
Mkazi wa IOM Dr. Qasim Sufi mara baada ya ufungaji wa vifaa hivyo.
…………………………………………………………..
Idara ya Uhamiaji katika Kituo
cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA)
imefunga Vifaa vyenye mfumo mpya wa utambuzi na ulinganisho wa sura
(Facial Recognition and Matching System) kwa abiria wanaoingia nchini.
Akiongea baada ya kupokea vifaa
hivyo, Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Divisheni ya Usimamizi na
Udhibiti wa Mipaka Samwel Rhobby Magweiga, amesema kuwa huo ni
muendelezo wa mikakati ya Idara katika kuimarisha na kuhuisha KANZIDATA
ya wanaoingia nchini.
“Vifaa na mfumo huu utasaidia
sana katika kukusanya taarifa za abiria wote wanaoingia nchini kupitia
hapa (JNIA), kama mlivyofahamishwa, mfumo huu unachukua sura ya mtu na
kulinganisha na sura nyingine zilizomo kwenye kanzidata ili kuhakikisha
taarifa zilizo kwenye pasipoti yake ni za pekee na hakuna mtu mwenye
sura kama yake au mtu mwenye sura ingine kuwa na taarifa kama
zake.”Alieleza Kamishna Samwel Magweiga.
Awali wakati akabidhiana vifaa
hivyo, Mwakilishi mkazi wa Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) Dr.
Qasim Sufi alisema kwamba IOM itashirikiana na Idara ya Uhamiaji katika
suala zima la udhibiti wa uingiaji na utokaji wa raia na wageni.
Idara ya Uhamiaji kwa
kushirikiana na shirika hilo, wamefunga vifaa vingine vyenye mfumo huo
kwenye vituo vya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA)
pamoja na mpaka wa Holili kwa pande zote mbili za Tanzania na Kenya.
Kupitia ushirikiano huo na IOM,
Idara ya Uhamiaji itaendelea kuimarisha maeneo yote ya mipaka kwa
kufunga vifaa na mfumo huu wa kisasa zaidi kutumiwa hapa Afrika
Mashariki.
Tags
Idara ya Uhamiaji