Wananchi wa Kata ya Mwakidete mtaa wa Mwakidete mkoani Mbeya wakiendelea na Usajili Vitambulisho vya Taifa.
Mmoja wa wananchi wa Mtaa wa
Mwakidete akiweka saini kwenye mashine maalumu ya uchukuliaji alama za
kibaiolojia, picha na saini ya kielektroniki.
Wanaoonekana kwenye picha ni
Baadhi ya Maafisa Usajili wa NIDA wakiendelea na zoezi la kuwasajili
wananchi wa Kata ya Mwakidete mkoani Mbeya. Kushoto ni Afisa Usajili
Wilaya ya Mbeya Bi. Alavuya Ntalimwa akitabasamu jambo na wananchi wa
Mtaa wa Mwakidete.
Mwananchi akichukuliwa alama za Vidole na afisa Usajili wa NIDA wakati zoezi la kuwasajili wanannchi likiendelea.
Msururu wa wananchi wa Mtaa wa Mwakidete wakisubiri huduma ya usajili.
…………………………………………………………………….
Mamlaka ya Vitambuisho vya Taifa
(NIDA) inaendelea na zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu mkoani Mbeya
ambapo wananchi wengi wamejitokeza ambapo kwa sasa usajili unaoendelea
niwa mkupuo (mass registration) ambapo wananchi wanakusanyika kwenye
mitaa na vijiji wanakoishi kusajiliwa ambapo Usajili huo unahusisha
ujazaji fomu, uchukuaji alama za vidole picha na saini ya kielektroniki.
Akitoa elimu kwa umma kuhusu
taratibu za Usajili mwakilishi wa kitengo cha Mawasiliano NIDA Bw.
Deodatus Alexander Mchaki amesema zoezi hilo ni fursa ya kipekee kwa
wananchi kutambuliwa na kusajiliwa.
Amesisitiza zoezi la usajili ni Bure
na wananchi hawatakiwa kutozwa gharama zozote Ili kusajiliwa mwananchi
ni lazima afike na nakala (photocopy) ya nyaraka/viambatisho vifuatavyo
kuthibitisha Umri, Uraia na Makazi yake ikiwemo cheti cha kuzaliwa,
Passport (Pasi ya kusafiria), Kadi ya kupigia kura, leseni ya udereva,
ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria na vyeti vya elimu.