Serikali ya nchini Zimbabwe kupitia Waziri wake mpya wa
kilimo , imeamuru kuridishwa kwa mashamba yaliyokua yakimilikiwa na
wakulima Wazungu, ambao walinyang'anywa wakati wa utawala wa Mugabe na
kupewa raia wa Zimbabwe.

"Wote ambao wamewekwa kinyume cha sheria katika mashamba ambayo si mali yao wanapaswa kuyarudisha haraka iwezekanavyo," alisema Perence Shiri, Waziri mpya wa Kilimo wa Zimbabwe siku ya Alhamisi.

Shiri alisema kuwa hatua hiyo inalenga kukuza kilimo kwa ajili ya uchumi wa nchi hiyo ambao unaendelea kudorora kila kukicha.
"Ikiwa tunataka kufanikisha malengo yaliyowekwa na serikali na kutumia kilimo kama nguzo ya uchumi, lazima tuhakikishe urasibu mzuri wa kilimo," waziri Shiri aliongeza.

Tags
Zimbabwe ya Mugabe