BANDA MEDIA BLOG

WAPALESTINA 4 WAPIGWA RISASI NA VIKOSI VYA ISRAEL



Israel: Wapalestina wanne wamepigwa risasi na vikosi vya Israel na wengine 150 wamejeruhiwa wakati wa mapambano katika ukingo wa magharibi na ukanda wa Gaza. Vifo hivyo vimetokea mnamo wakati maelfu ya Wapalestina wakiendelea na maandamano dhidi ya uamuzi wa Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Polisi wa Israel wamesema afisa mmoja amechomwa kisu na kujeruhiwa jirani na kituo cha upekuzi barabani nje kidogo ya mji wa Ramallah. Wapalestina ambao wanadai Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu wa taifa lao la baadaye wanasema uamuzi huo wa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel unaifanya Marekani kutokuwa na jukumu lolote kama mpatanishi wa mazungumzo ya amani yaliyokwama.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG