LIGI Kuu Tanzania Bara raundi ya 12 inatarajiwa kuendelea
siku ya Jumapili ambapo miongoni mwa michezo itakayochezwa siku hiyo ni
mabingwa watetezi Yanga watakaopambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza. Mechi nyingine ni Njombe Mji na Singida United.

Akizungumzia mchezo huo wa Jumapili, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema: “Tunajua Mbao ni timu ambayo imejiandaa kukutana na sisi mabingwa watetezi, hivyo tunahitaji ushindi na hata wao wanahitaji ushindi.
Kikubwa ni kwamba tumejiandaa kushinda licha ya kwamba tumekuwa hatuna matokeo mazuri tunapokutana nao.
“Vijana wetu wako vizuri na leo timu yetu imeingia jijini Mwanza na kesho Jumamosi itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa ni siku moja kabla ya mechi.
“Katika mchezo huo tunatarajia kuwakosa Ibrahim Ajib ambaye ana kadi tatu za njano, Beno Kakolanya ambaye yupo Mbeya akimuuguza mama yake, na Obrey Chirwa ambaye yuko Zambia.”

Tags
YOUNG AFRICAS