
Beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji ameiandikia barua klabu yake akitaka imuachie aende zake kutafuta maisha.
Haji ameindika barua akitaka Yanga imuachie aende kujiunga na klabu ya AFC Leopards ya Kenya ambayo tayari kumsajili.
Akizungumza
na SALEHJEMBE, Haji amesema ameona hana nafasi ya kucheza katika kikosi
cha Yanga, hivyo angependa kwenda kujiendeleza zaidi.
"Kama
sina nafasi, maana yake sina msaada na sihitajiki. Hivyo kwa
makubaliano mazuri bila ya kugombana acha niende nikajiendeleze.
"Kazi
yangu ni soka na ninataka kujiendeleza. Siwezi kuendelea nikiwa benchi,
hivyo Yanga nimewaandikia waniachie niwahi kujiunga na AFC Leopards,"
alisema.
Beki
huyo alionyesha kiwango cha juu na kuisaidia Zanzibar Heroes kufika
fainali ya Kombe la Chalenji lililomalizika wiki moja na ushee
iliyopita.
Tags
MWINYI HAJI