BANDA MEDIA BLOG

Ufafanuzi kuhusu kauli ya Rais wa TFF juu ya mashindano ya Ndondo


Nimefuatilia kwa karibu na kwa umakini mkubwa sana mijadala na maoni ya wadau mbalimbali wa soka mara baada ya kauli ya Rais wa TFF Wallace Karia hapo jana kutangaza kufuta mashindano yoyote ambayo yapo nje ya mfumo washirikikisho hilo isipokuwa kwa kibali maalum.

Karia amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kupata malalamiko mengi kutoka kwa viongozi wa ngazi za wilaya na mikoa kuwapo kwa mashindano ambayo yanaendeshwa kiholela huku yakiwa hayaheshimu taratibu za mpira.
“Nimepata malalamiko mengi kutoka kwa viongozi wetu ngazi za wilaya na mikoa kwamba kuna mashindano yanayoendeshwa kiholela halafu ni mashindano ambayo hayahesimu taratibu za mpira yanachafua mpira wetu lakini pia yanatumia baadhi ya waamuzi ambao tumewafungia pamoja na viongozi wengine ambao wametuhumiwa kwa mambo mbalimbali hawapo tena kwenye uongozi kwa hiyo wanakuja kwa mlango wa uwani”-Wallace Karia.
“Pia tuaangalia haya mashindano lazima yawe na tija, sasa ili hiki kitu kiweze kuwa na tija wale wadau ambao wameamua kusaidia mpira lakini wengine wanasababu zao basi nia na sababu zao ziungane na za kwetu ili kuendeleza mpira uwe na tija.”
“Tunatengeneza taratibu na vigezo ambavyo anaeyetayarisha mashindano anatakiwa akidhi vigezo hivyo, endapo atakidhi vigezo, ngazi husika wilaya au mkoa itaruhusu hayo mashindano.”
Naomba kuliweka sawa jambo hili kwa wadau, niwakumbushe kidogo kuwa, fainali ya Ndondo Cup Dar 2017 ilihudhuriwa Mkurugenzi wa FIFA Bw. Veron Mosengo anayehusika na maendeleo ya soka la Afrika pamoja na nchi za Caribean.
Mosengo alifurahishwa sana na Ndondo Cup na alimuomba Rais Karia kuona namna TFF inavyoweza kusaidia mashindano hayo kuwa makubwa zaidi, moja ya vitu alivyoshauri ili mashindano hayo yaweze kutambuliwa na FIFA ni kushirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 23 (U23).
Hivi karibuni nilikutana na tena na Bw. Mosengo jijini London kwenye sherehe za tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia, katika mazungumzo yetu hakusahau kunigusia namna ofisi yake yaani FIFA itakavyo saidia Ndondo Cup kupitia TFF.
Mara kadhaa nimezungumza na Kaimu Katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao, ameniambia namna TFF ilivyodhamiria kusaidia mashindano hayo (Ndondo Cup) mwakani hasa katika upande wa ufundi.
Kwa hiyo ndugu zangu, Ndondo Cup ipo na itaendelea kuwepo bila tatizo lolote huku ikiendelea kupata baraka zote za mamlaka zote za mpira wa miguu hususan vyama vya mikoa. Kwangu naona fursa kubwa zaidi kwa Ndondo Cup kutambulika na TFF itaturahisishia sisi waandaji kupenyeza agenda yetu  ya Ndondo Cup kirahisi kuvuka mipaka kwa mashirikisho mengine barani Afrika.
#NdondoCup2017Waleteee

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG