BANDA MEDIA BLOG

TIMU YA BUNGE LA TANZANIA YA MPIRA WA MIGUU YAITANDIKA TIMU YA BUNGE LA BURUNDI 3-1


pic a
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na Kocha wa Timu wa ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Venance Mwamoto wakati alipokuwa akiwasalimia Wachezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania na Wachezaji wa Bunge la Burundi kabla ya kuanza kwa mechi baina ya timu hizo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Bunge la Tanzania ilishinda kwa mabao 3 – 1. Mechi hiyo lilichezwa ikiwa ni sehemu ya Mashindano ya Kimichezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika yalioanza mwishoni mwa wiki na yanatarajiwa kwisha tarehe 10 Desemba, 2017.
pic b (1)
Mshambuliaji wa Timu ya Bunge la Tanzania Mhe. Ridhiwan Kikwete akiwatoka Mabeki wa Timu ya Bunge la Burundi wakati wa mechi baina ya timu hizo ikiwa ni sehemu ya Mashindano ya Kimichezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika yalioanza mwishoni mwa wiki na yanatarajiwa kwisha tarehe 10 Desemba, 2017 ambapo Timu ya Bunge la Tanzania ilishinda kwa mabao 3-1.

pic b (3)
Mshambuliaji wa Timu ya Bunge la Tanzania Mhe. Ridhiwan Kikwete akipiga  mpira kuelekea katika Lango la Timu ya Bunge ya Burundi wakati wa mechi baina ya timu hizo ikiwa ni sehemu ya Mashindano ya Kimichezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika yalioanza mwishoni mwa wiki na yanatarajiwa kumalizika tarehe 10 Desemba, 2017 ambapo Timu ya Bunge la Tanzania ilishinda kwa mabao 3-1.
pic d
Kikosi cha Timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika picha ya Pamoja kabla ya kuanza kwa mechi yao na Timu ya Bunge la Burundi ambapo walishinda 3-1

PICHA NA BUNGE

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG