BANDA MEDIA BLOG

Faida za Mapinduzi Cup kwa Yanga


Wakati wadau kibao wakibeza mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea visiwani Zanzibar wakitaka wachezaji wanaotoka ligi kuu Tanzania bara kupumzishwa, kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa yupo tofauti nao kabisa akimiani kuwa mashindano hayo yatawasaidia wachezaji wake kuimarika katika kipindi hiki cha mashindano hayo.

“Kuna umuhimu wa mashindano ya Mapinduzi kwenye kikosi chetu kwa sababu tunawachezaji wengi walikuwa wanauguza majeraha, wengine walikuwa hawapati nafasi mara kwa mara wengine wapya lakini pia tuna vijana ambao tunahitaji kuwa nafasi kwa hiyo ni wakati wa kuboresha kikosi chetu katika mashindano haya”-Shadrack Nsajigwa.
Nsajigwa hakutaka kuongelea kama kuna uwezekano wa Ngoma, Kamusoko, Ajib na Yondani kuungana na wachezaji ambao wako Zanzibar kwa ajili ya kombe la Mapinduzi.
Leo Jumanne January 2, 2018 Yanga itacheza mchezo wake wa kwanza wa Mapinduzi Cup mwaka huu dhidi ya Mlandege saa 2:15 usiku kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG