BANDA MEDIA BLOG

“Nahitaji msamaha wenu mashabiki, viongozi na benchi la ufundi”-Juma Mahadhi


Kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi ameandika ujumbe mrefu kwenye mtandao wake wa Instagram (@jumamahadhi21) akiomba msamaha mashabiki, viongozi na benchi la ufundi.
Mahadhi hajaweka wazi kitu gani kimetokea hadi ameamua kuomba msamaha huo wakati huu wa sherehe za mwaka mpya 2018.

“Asalam alykum ndugu zangu katika imani haja yangu ni kuomba radhi kwa mashabiki wangu wote na wapenzi wote wa mpira wa miguu duniani, nakiri kufanya makosa hapo nyuma na nimejifunza mengi kupitia nyinyi nawaomba radhi.”
“Haja ya moyo wangu ni kutaka kufikia malengo yangu niliyojiwekea lakini kwa mwaka huu ilikuwa ngumu sana kutokana na changamoto nilizokutana nazo.”

“Sasa ombi langu kwenu mashabiki, viongozi na benchi la ufundi ni kwamba nahitaji msamaha kama niliwakosea bado nahitaji nafasi naamini siwezi kurudia kosa kwani nimejifunza mengi naahidi kuwa Mahadhi mpya naomba imani yenu kwangu kama mnaona bado nahitajika katika timu yangu pendwa Yanga SC.”

“Tumaini langu kilio change kimewafikia nahitaji sasa kuanza mwaka mpya nikiwa kijana mwema na mpya. Asanteni sana nawapenda wote.”

Mahadhi amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga, mwezi May 2017 zilisambaa tetesi kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Coastal Union huenda angetolewa kwa mkopo kwenda Singida United lakini yeye alisema, ni bora aondoke jumla kuliko kutolewa kwa mkopo.
Ni kipindi hichohicho pia Mahadhi alisema kulikuwa na ofa kadhaa kutoka vilabu vingine vya VPL na nje ya nchi vikihitaji huduma yake lakini hakuwa tayari kuvitaja kwa sababu ya mkataba alionao na mwajiri wake wa sasa Yanga.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG