BANDA MEDIA BLOG

WAFANYABIASHARA WA VIUMBEPORI HAI WAMCHANA ALIYEKUWA WAZIRI JUMANNE MAGHEMBE .

 Zuio la biashara ya viumbepori hai lililofanywa na serikali limezua sintofahau kwa wafanyabiashara wa Viumbepori hai ikiwemo kukosa kodi ya nyumba pamoja na watoto kushindwa kwenda shule.

Akizungumza kwenye kikao cha wizara ya maliasili na utalii na wawakilishi wa wafanyabiashara wa viumbepori hai kilichofanyika Leo mjini hapa makamu mwenyekiti wa TWEA Fatuma Hamisi amesema zuio hilo limeleta athari nyingi ikiwa ni pamoja naukosefu wa mitaji kwa wafanyabiashara kumepelekea watoto kushindwa kwenda shule kwa sababu baadhi ya wazazi au walezi walikuwa wanasomesha watoto wao kwa kutumia biashara hiyo.

Aidha amesema kumzuia mtu bila kufuata taratibu za kisheria hii inasababisha kuathiri mfumo wa maisha na taifa kukosa maendeleo.    [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]



Hata hivyo ameongeza kuwa miongoni mwa athari zingine ni pamoja na watu kukosa kipato na kuleta ukosefu wa ajira nchi.


Akizungumzia zuio hilo Hamisi amesema zuio hilo lilifanywa kinyume na taratibu za kisheria kwani halikufuata sheria na kanuni zilizopo ikiwemo kutoa taarifa kwa wafanyabiashara husika.

Amesema mahakama katika hukumu yake iliwakuta watuhumiwa hao wa mh. Jumanne Maghembe hawakuwa na hatia yeyote kwani walikuwa wamefuata misingi na taratibu za kisheria katika biashara hiyo
Mbali na hayo ameiomba serikali ifungue zuio hilo , leseni za uwindaji wa mamba kwa wazawa zirejeshwe, leseni zitolewe upya bila malipo na wafanyabiashara wote wa viumbepori hai wasipewe huduma bila kuwa wanachama wa TWEA ili kuwa na uwakilishi mpana na kuondoa mkanganyiko uliopo leo ili kujenga taswira yenye weledi.

Naye mwenyekiti wa mashamba ya kuzalisha viumbepori hai Paul madinda amesema wizara take ilikuwa na wafanyakazi 24 na shamba hekta 80 mpaka sasa wamebaki wafanyakazi wane kutokana na kushindwa kuwalipa mishara jambo linalopelekea maisha yao kuyumba nakuleta umasikini katika kaya.
Naibu waziri wa maliasili na Utalii Japhet Hasunga amewataka wafanyabiashara hao kuwa na subira wakati serikali inafanya utaratibu wa kutatua tatizo hilo.

 
Biashara ya kusafirisha viumbepori hai ilizuia ghafla tarehe 17 machi 2016 na aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii professa Jumanne Maghembe baada ya tukio alilofanya la kukamata ngedere uwanja wa Kilimanjaro (waliokuwa wakisafirishwa isivyo halali) bila kuwa na wataalamu wa wizara.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG