BANDA MEDIA BLOG

WATU 4 WANASWA DOM NA NYARA ZA SERIKALI.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akiwaonyesha waandishi wa habari watuhumiwa wa makosa mbalimbali ambao jeshi hilo limewakamata wiki ya kwanza ya mwaka 2018

Hapa akionnyesha baadhi ya pikipiki zilizokamatwa mjini Dodoma zikiwa katika matukio ya kiuharifu

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akionyesha Ngozi za Chui ambazo jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa 4 wakifusishwa na ujangiri huo Wilayani Kongwa [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]


Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limewakamata watu wanne wakiwa na nyara za serikali ambazo ni ngozi nzima tatu pamoja na vipande sita za mnyama wa porini aina ya Chui katika kijiji cha Mkoka kata y a Mkoka, Tarafa ya Zoissa wilaya ya Kongwa Mkoani hapa.


Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoani Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe mwezi wa nne mwaka huu majira ya saa tano asubuhi huko katika kijiji cha mkoka kata ya mkoka ,Tarafa ya zoissa wilayani kongwa.

Muroto amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na nyara hizo wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo MOSCOW katika chumba namba tano pia ameeleza watuhumiwa walikuwa katika nyumba hiyo ya kulala wageni kwa lengo la kumsuburi  mnunuzi wa ngozi hizo ambazo ni nyara za serikali zenye thamani ya 95,000,00.


Kamanda huyo amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Yohana Tibu mwenye umri wa miaka 35 mkulima mkazi wa zoissa wilayani kongwa, Abdallah Mwana mwenye umri wa miaka 34 mkuima mkazi wa kijiji cha chitego kongwa.


Wengine ni Emmanuel Hurdson,mwenye umri wa miaka 30 mkulima mkazi wa idobo morogoro pamoja na Suzana Shauri ,mwenye umri wa miaka 35 mkulima mkazi wa zoissa wilayani kongwa mkoani Dodoma.


Katika tukio lingine jeshi la polisi limewakama watu sita wakiwa na pikipiki mbili MC 950 ALT FEKON na MC 538 BPK SANLG ambazo lzilikuwa zikitumika katika vitendo vya ukabaji na uporaji amewataja watu hao kuwa ni Charles Paul Isinyika mwenye umri wa miaka 22 Gabriel Nehemia mwenye umri wa mika 27 Seleman Juma Muando mwenye umri wa miaka 30 Mashaka Lutawandu mwenye umri wa miaka 26,na Festo Petro mwenye umri wa miaka 25 pamoja na Maulid Said mwenye umri wa miaka 19 wote ni wakazi wa mkoa wa Dodoma.


Jeshi la polisi mkoani humo linaendelea na uchunguzi wa matukio yote na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika pia ametoa wito kwa watu wakubali kubadilika na wafanye kazi halali uhalifu haulipi na Dodoma siyo Sehemu salama kwa wahalifu.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG