Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Amani Abeid Karume ilyopo kata ya Pahi wilayani Kondoa wameandamana hadi
ofisini kwa mkuu wa wilaya hiyo Sezaria Makota wakidai kupewa Adhabu za
kuchimba visiki, na vibarua vya kushusha mizigo ya ujenzi wa shule
jambo ambalo linawakatisha masomo yao.
Hayo yamebainika wakati mkuu huyo
wa wilaya akiongea na wanafunzi hao kwenye ukumbi wa Kondoa Irangi na
kutoa Agizo la wanafunzi hao kurejea shuleni wakati malalamiko yao
yakiendelea kutatuliwa na mwisho wake ni jumamosi ya wiki hii yote
yatakuwa yameshughulikiwa.
Amesema kuwa malalamiko
waliowasilisha ofisini kwake na viongozi wa wanafunzi hao ni pamoja na
kukosa huduma sahihi za afya ikiwemo kutokuwepo kwa dawa kwenye kituo
cha Afya Pahi na kadi za CHF za wanafunzi wengine kutofanya kazi,pia
kupewa Adhabu ya kuchimba visiki wakati wa masomo.
Mkuu huyo wa wilaya Amebainisha
kuwa uonevu kwa wanafunzi hao ni marufuku ambapo akawataka Afisa elimu
kuhakikisha kunakuwepo na Box la maoni shuleni hapo sanjari na kuchukuwa
hatua za kinidhamu kwa wale wote watakaokaidi Agizo hilo.
“Nawataka watoto wangu kubwa ni
nidhamu ila mwende shule wakose sababu na mbadilike kwani watawatafutia
sababu ila malalamiko yenu mpaka jumamosi mabadiliko mtayaona na
tunaendelea kuyafuatilia kwa ukaribu nami ntafika shuleni hapo wakati
wowote wiki hii” alisema dc
Miongoni mwa malalamiko ya
wanafunzi hao ni matibabu hafifi,kadi za CHF hazifanyikazi,kupewa adhabu
za kuchimba visiki wakati wa masomo, kulipia Nembo ya shule hadi sasa
hawajapewa, makamu wa mkuu wa shule kumpiga mwanafunzi teke na michango
iliyopitiliza ikiwemo kutakiwa kulipia rimu 8 kwa ajili ya majaribio na
mitihani.
Amesma kuwawaraka wao ameoupokea
na atahakikisha anaufanyiakazi haraka iwezekanavyo na kumuagiza
mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kondoa Vijijini kuhakikisha
wanafunzi wote waliofika ofisini kwake na wale 7 walioshindwa kufika
ofisini kwake wanafika salama shuleni na wasibugudhiwe na waendelee na
masomo yao.
DC Makota amewataka waalimu wote
ambao hawaingii Darasani kuingia mara moja kufundisha,huku akisema kuwa
wanafunzi hao ni marufuku kufanya vibarua vya kubeba mizigo ya ujenzi wa
majengo na kumtaka pia mkurugenzi kuhakikisha wanafunzi saba waliobakia
njia kama wapo salama
Tags
ELIMU