Halmashauri ya Bahi mkoani Dodoma imeadhimisha
sherehe za siku ya wanawake duniani kwa kufanya usafi na kupanda miti
katika kata ya Ibihwa wilayani humo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya hiyo Elizabeth Kitundu amesisitiza suala la wanawake kujitambua ili waondokane na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi yao na waweze kujikwamua kiuchumi.
"Wanawake tunakumbana na vitendo vingi vya unyanyasaji, tusipoamka vitendo hivi vitarudisha nyuma jitihada zetu za kututoa hapa tulipo,"alisema mkuu huyo.

Alitoa agizo la kusakwa kwa wanafunzi wa kike 72 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ambao hawajaripoti shuleni mpaka sasa.
"Sambamba na kutafutwa kwa wanafunzi hawa pia wote waliosababisha wanafunzi hawa watafutwe pia na kuchukuliwa hatua,hao na watoto wa kike lakini pia wapo wanafunzi wa kiume 39 nao hawajaripoti watafutwe popote walipo waripoti shuleni,"alisisitiza Kitundu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Rachel Chuwa amewataka watoto kujitambua na kutokubali kurubuniwa kwa kuwa matokeo ya hayo ni kukatisha ndoto zao walizokuwa nazo.

"Wazazi wenzangu tushirikiane tusifiche vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto wetu, tushirikiane na vyombo vya dola tuwafichue ili kukomesha vitendo hivi,"alisema mkurugenzi huyo.

Tags
DC BAHI