Jugnauth aliyasema hayo jana Ijumaa huko Port Louis, mji mkuu wa kisiwa hicho kilichoko katika bahari ya Hindi na kubainisha kuwa, sakata la ufisadi wa kifedha linalomsakama rais huyo limemsukuma ukutani na hana chaguo jingine ila kujiuzulu.
Amesema, na hapa tunanukuu, "Tumekubaliana na rais kuhusiana na yeye kujiuzulu na hata tarehe ya kuachia ngazi." Hata hivyo Waziri Mkuu huyo wa Mauritius alikataa kuwaambia waandishi wa habari kuhusu tarehe ya kujiuzulu rais.
Vyanzo vya habari nchini humo vimefichua kuwa rais huyo atajiuzulu rasmi Jumatatu ijayo ya Machi 12, baada ya nchi hiyo kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake.
Gurib-Fakim mwenye umri wa miaka 58 amekuwa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya kisiwa hicho, tokea mwaka 2015.
Tags
UFISADI