Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk .John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
zoezi la kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa reli ya kisasa (standard
gauge) Mkoani Dodoma.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo mjini hapa.ambapo amesema zoezi hilo litafanyika marchi 14 mwaka huu katika eneo la Ihumwa.
Hata hivyo Dk Mahenge amesema kuwa mradi wa reli hiyo ya kisasa kutoka Dar es salaam hadi mwanza ambao ni kilometa 1219 umegharimu takribani Tilioni 15.
Akiendelea kufafanua zaidi Amesema kutoka Morogoro hadi Dodoma ambapo ni kilometa 522 mradi unagharibu takribani Tilioni 7,hivyo anampongeza Raisi kwa juhudi anazozifanya.
Aidha amesema kuwa TPA wameanza ujenzi wa kujenga bandari kavu ambapo itakua msaada kubwa kwa mikoa ya jirani kama Mwanza na Singida kuweza kushusha mizigo yao katika bandari hiyo.
Amesema kuwa ujenzi wa reli ya kisasa utasaidia kuzalisha ajira kwa vijana wenye elimu na wasiokuwa na elimu hivyo aliwahimiza wananchi mkoani hapa kuchangamkia fursa hizo.
"Mradi huu utatoa ajira kwa vijana wengi pia utakapokamilikawa utafanya mkoa wetu uwe wa kuvutia wawekezaji na watu mbalimbali wanaohitaji kuja," amesema Dk Mahenge.
Dk Mahenge amesema kuhusu ujenzi wa stand mpya ya kisasa utaanza mwezi April mwaka huu ambao utaambana na ujenzi wa soko la kisasa.
Hata hivyo mbali na uwekaji wa jiwe la msingi wa reli unatarajiwa kumalizika ifikapo mwaka 2020.

Tags
STANDARD GAUGE