BANDA MEDIA BLOG

UHABA WA FEDHA WAIKUMBA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.


Wizara ya Ujezi, Uchukuzi na Mawasiliano inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa fedha na kusababisha baadhi ya sekta kushindwa kufanya kazi zake ipasavyo.

Hayo yalielezwa jana na katibu mkuu wa wizara hiyo Dk Maria wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) lililofanyika mjini hapa.
Dk Sasabo alisema kutokana na uhaba wa fedha sekta ya mawasiliano imeshindwa kujitangaza ipasavyo na kusababisha baadhi ya watukutokuwa na uelewa juu ya masuala mbalimbali.
“Jamii ya watanzania pamoja na baadhi yetu hapa bado ina uelewa mdogo juu ya masuala mbalimbali ya sekta ya Mawasiliano,hivyo elimu zaidi inahitajika kwa Umma kwa kutumia njia zilizopo ili kuelimusha jamii kuhusu maana na umuhimu wake ili tufikie malengo yetu na kwa kasi ya kutosha”alieleza Dk Sasabo.

Akifafanua zaidi Katibu huyo alisema miongoni mwa changamoto nyingine ni pamoja na ukosefu wa fedha za miradi ya maendeleo na matumizi mengine kushindwa kufika kwa wakati.
Akiendelea kufafanua alisema kutokana na hali hiyo imesababisha kutokamilika kwa baadhi ya shughuli zilizopangwa.
“Hivyo zinahitajika juhudi za makusudi zifanyike za kupata fedha ili shughuli zilizopangwa kufanyika ziweze kutekelezwa kwa ukamilifu” alisisitiza.
Mbali na hayo kaitbu huyo alitoa rai na kuwataka wakuu wa idara na vitengo kutekeleza majukumu kwa ufanisi kwa kutoa huduma bora kwa kuzingatia vigezo walivyojiwekea.
“Kama mnavyojua serikali kupitisa Wizara inapimwa kutokana na namna inavyotekeleza majukumu yake kwa wananchi kwa ufanisi.
“Mkiwa kama wajumbe wa baraza la sehemu muhimu sana ya wafanyakazi wa sekta yetu ni vyema mkaonyesha kwa mfano katika kufanya kazi na kutekeleza majukumu yenu hii itasaidia sana katika kuhamasisha watumishi wengine kufanya kazi kwa bidii na ufanisi mkubwa ”aliongeza kwa kusemaDk Sasabo.
Kwa upande wake mwanasheri wa Sekta ya Mawasiliano,Eunice Masigah akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa baraza hilo alisema baraza hilo litawezesha wajumbe kutambua umuhimu wa mawasiliao katika njia endelevu na za uzalisha.
Pia alisema kuwa kwa sasa juhudi za kupambana na watu ambao wanatumia vibaya mitandao zinaendelea ikiwa ni pamoja na kutambua vyema sheria ya makosa ya mitandao.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG