BANDA MEDIA BLOG

UFAHAMU UMRI WA KUFANYA MAPENZI KATIKA NCHI MABALI MBALI



Paris: Kila nchi Duniani inaumri wake sahihi wa vijana kuanza kushiriki kufanya mapenzi na umri huo unawekwa kwenye kaitba kama Sheria Rasmi, sasa nchini Ufaransa inatarajia kuweka sheria maalum ya umri wa kuanza kufanya mapenzi kuwa ni miaka 15.Hivyo kufuatia mapendekezo hayo mtu yeyote atakabainika kufanya mapenzi chini ya umri huo atakuwa amebaka.

Maamuzi haya yamekuja nchini humo mara baada ya madaktari na wanasheria kutoa ushari wao kuhusiana na umri unaostahili kuanza kufanya mapenzi.
Mabadiliko haya yamekuja kufuatia kesi mbili za hivi karibuni nchini Ufaransa zilizohusisha wanaume waliofanya mapenzi na wasichana waliokuwa na umri wa miaka 11.

Katika sheria ya sasa kama mtu amekutwa na kosa la kufanya mapenzi na mtu chini ya miaka 15 iwe kwa hiari ama makubaliano,mshtakiwa atahukumiwa kwa kosa la kujamiana na mtoto lakini sio kosa la ubakaji. Kosa hilo litamlazimu mshtakiwa kutoa kiasi cha dola 87,000 kama sehemu ya adhabu na kwenda jela miaka mitano.


Huu ndio umri sahihi wa kushiriki kufanya mapenzi katika nchi mbalimbali Duniani
Austria,Ujerumani,Italia ni miaka 14
Ugiriki, Poland, Sweden ni miaka 15
Ubeligiji, Netherland, Spain, Urusi na Uingereza ni miaka 16


Barani Afrika
Miaka 12;Angola
Miaka 13; Burkina Faso, Comoro, Niger
Miaka 14;Botswana (wanaume), Cape Verde, Chad (wasichana), Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wasichana), Lesotho (wanaume), Madagascar na Malawi
Miaka 15; Guinea, Morocco

Miaka 16 ni Algeria, Botswana (wanawake), Cameroon, Ghana, Guinea Bissau, Lesotho (wanawake), Mauritania, Mauritius, Mozambique, Namibia, Senegal, Afrika kusini, Swaziland, Togo, Zambia, Zimbabwe.
Miaka 18;Benin, Burundi, Afrika ya kati,Ivory Coast, DRC (wanaume), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gabon, Gambia, Kenya, Liberia, Mali, Nigeria, Republic of Congo, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Somalia, South Sudan, Tanzania, Uganda.
Miaka 20;Tunisia

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG