Waziri mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
amesema viongozi wanatakiwa kuwa waadilifu na wachamungu badala ya
kufanya kazi kwa ubinafsi,chuki na kula rushwa.

Pinda ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifunga kongamano la Maombi ya kuliombea taifa pamoja na viongozi kwa kuratibiwa na Kingdom Leadeship Netwark Tanzania lililofanyika mjini Dodoma .
Pinda amesema kuwa ili uweze kuwa na Taifa lenye viongozi wazuri wasihojihusisha katika vitendo vya rushwa na kuwa na utawala bora ni lazima kupata viongozi ambao ni wacha Mungu na wenye hofu ya kimungu.
Kwa upande wake kiongozi aliyekuwa makamu wa benki ya dunia kanda ya Afrika, Dk.Oby Ezekwesili kutoka nchini Nigeria akitoa mada katika kongamano la maombi juu ya utawala bora,uwazi na uwajibikaji amesema kuwa ili nchi iweze kusonga mbele ni lazima kuwa na viongozi ambao wanazingatia misingi ya utawala bora.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo aliimiza utoaji wa elimu juu ya kutunza Maliasili za nchi huku suala zima la uzalishaji likipewa kipaumbele kwa njia ya kutunza vyanzo vyote vya mapato ikiwa ni pamoja na kujiepusha na masuala ya rushwa,ufisadi na ubadhilifu wa mali ya Umma.
Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr.Binilith Mahenge amepongeza kuanzishwa kwa kongamano hilo nakutaka liwe endelevu kwa manufaa ya taifa.
Isack Mpatwa ambaye ni mkurugenzi wa Kingdom Leadeship Netwark Tanzania akitoa utambulisho wa kongamano hilo,amesema kuwa lengo kubwa la kuwakutanisha viongozi wa kitaifa na kimataifa ni kutaka kufikisha kwa urahisi dhana ya utawala bora kwa watendaji pamoja na kumshirikisha mungu katika utawala wa taifa na viongozi kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa kuzingatia utawala bora na wa kisheria,kuliombea taifa na kumshukuru mungu kulilinda taifa.

Tags
PINDA