Bango linaloonyesha msitu wa hifadhi ya Taifa ya Uzigua.
Ofisa msaidizi wa misitu
Bagamoyo,Jonathan Mpangala,akionyesha mipaka ambayo imewekwa katika
msitu wa hifadhi ya Taifa Uzigua ,wakati mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi
Evarist Ndikilo (wa katikati mwenye suti)alipotembelea msitu huo
Mkuu
wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo (mwenye suti nyeusi)
akitembelea msitu wa hifadhi ya Taifa Uzigua ,Wa kushoto ni mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo ,alhaj Majid Mwanga.
Picha na Mwamvua Mwinyi
………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi
Evarist Ndikilo ,amekemea wenye nia ya kuvamia msitu wa hifadhi -Uzigua
wilayani Bagamoyo na atakaethubutu kufanya hivyo tena atakiona.
Aidha ,ameutaka wakala wa misitu
kanda ya Mashariki na wilayani hapo ,kuendelea kukaza uzi katika kufanya
doria mbalimbali ili kudhibiti uvamizi uliokuwepo kipindi cha nyuma .
Akizungumza wakati alipokwenda
kutembelea msitu wa Uzigua ,kujiridhisha kama umeanza kurejesha uoto
wake wa asili ,Ndikilo aliwaasa wananchi wakiwemo wafugaji kuheshimu
mipaka iliyopo na kuulinda msitu huo.
Alieleza kuwa ,mwaka mmoja
uliopita serikali ilifanya operesheni kali ambapo waliondoa kaya zaidi
ya 500 na maboma ya mifugo ya ng’ombe.
Hata hivyo Ndikilo alisema
,kwasasa kumewekwa vigingi vidogo na vikubwa kama mipaka vinaoonyesha
upande wa msitu na upande wa wananchi hivyo wasiendelee kuingilia mapito
ya njia zinazopita msituni humo na msitu wenyewe.
“Kuna watu walivamia na wengine
kuanza kuishi, kuvuna mbao, kukata miti kwa ajili ya mkaa, kuni ,kufuga
ng’ombe, kilimo, uchimbaji wa madini,na kusababisha athari kubwa kwa
msitu ”
“Msitu huu ni eneo la maji
yanayoingia mto Wami, tuliondoa watu wote ,na leo nimepita
nimejiridhisha ,nimeona wanyama wameanza kurejea, wanyama wana njia zao
hususan tembo ,tumeona wameanza kupita kwenye mapito yao kuelekea
Wamimbiki,Saadan,;”
“Miti imeanza kuota ,hivyo uoto wa
asili unajirudia kama zamani, hivyo jamii ikiiona inafukuzwa katika
misitu ijue misitu ina manufaa kwao ” alisema Ndikilo.
Mkuu huyo wa mkoa alichukua fursa
hiyo kuiomba jamii iheshimu na kuilinda misitu ya Uzigua ,Kazimzumbwi
-Kisarawe,Ruvu Kusini na Wamimbiki ambao wanapakana na Morogoro.
Nae mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
,alhaj Majid Mwanga,alisema tatizo lililopo ni muingiliano wa mifugo
hali inayosababisha wakulima kujiona kama wanabaguliwa .
Alielezea ,tayari wamekaa katika vikao vyao wameomba fedha kwa ajili ya kuondoa wafugaji watakaokaidi .
Alhaj Mwanga alisema, iifikie
hatua jamii ikawa na uelewa wa makusudio ya serikali yao na kuachana na
tabia ya kutaka kuhalalisha mambo yasiyokuwepo.
Ofisa msaidizi wa misitu
Bagamoyo,Jonathan Mpangala,alisema msitu huo ulitangazwa na serikali kwa
tangazo namba 466 ,la mwaka 1958.
Alisema kuna wilaya tatu
zilizoingilia msitu huo ikiwemo vijiji nane vya wilaya ya
Bagamoyo,vijiji viwili wilaya ya Kilindi na Handeni ni kijiji kimoja .
Mpangala alisema wakala wa misitu
ulipoanza mwaka 2014 ndipo msitu wa Uzigua ulipimwa tena rasmi ,ukiwa na
ukubwa wa hekta 24,436 ama kwa tafsiri ya hekari 61,090 ambako katika
kipindi hicho walitoa tangazo la kuwataka wavamizi waondoke.
Kwa mujibu wa Caroline Marundo kutoka TFS Kanda ya Mashariki, alimhakikishia mkuu wa mkoa ,kuwa msitu upo shwari .
Alisema hali inaridhisha kwani hakuna usumbufu wa watu kufanya shughuli zozote za kijamii.
Tags
MISITU