BANDA MEDIA BLOG

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO

Pix 1 Mwenyekiti Zungu
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Mussa Zungu akiongoza kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Pix 2 Mhe.Mwanjelwa
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt Mary Mwanjelwa akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa zao la korosho  linaendea kuwanufaisha wakulima Bungeni Jijini Dodoma.
Pix 3 Mhe.Mhagama na Mboni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe.Mboni Mhita  wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.

Pix 4 Mhe Mabula
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akitolea ufafanuzi tofauti iliyopo kati ya shule za Serikali na Binafsi na kusisitiza kwamba mitaala ya kimataifa imeruhusiwa ili kukidhi mahitaji ya raia wa kigeni wanaoishi nchini.
Pix 5 Mhe.Mpango na Bulaya
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt.Philip Mpango akizungumza jambo na Mbunge wa Bunda Mjini wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Pix 6 Mhe.Ngonyani
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Jacqueline Ngonyani akiomba ufafanuzi kwa Serikali kuhusu ulipaji wa Mawakala wa pembejeo wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Pix 7 Spika na jaji
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiwasalimie wabunge wakati wa utambulisho wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof Ibrahim Juma (kushoto)  wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Picha zote na Daudi Manongi, DODOMA

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG