Kipa wa zamani wa Simba na Timu
ya Taifa ya Tanzania, Juma Kaseja ‘Tanzania One’ leo Jumamosi
amewatibulia Simba baada ya kuivuruga rekodi yao ya kutaka kumaliza Ligi
Kuu ya VPL na kuchukua Ubingwa bila kupoteza mchezo baada ya kukamata
penati Okwi na kuwafanya Kagera kutoka na ushindi wa bao 1-0 katika
dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Kaseja amedaka penalti ya Okwi
katika dakika za nyongeza hivyo Kagera Sugar kuvunja rekodi ya kuwa timu
ya kwanza kuwafunga Simba kwa msimu huu baada ya kupachika bao dakika
ya 86 ya mchezo na kuibuka na pointi tatu hivyo kujikusanyia jumla ya
Pointi 34.
Awali kabla ya mchezo kuanza
Nyota wa Kagera Sugar walisema kuwa licha ya kwamba wapinzani wao
wameshatwaa Ubingwa, lakini watahakikisha wanashinda mchezo huo ili
kuwatibulia sherehe yao jambo ambalo wamefanikiwa kulitimiza.
Timu ya Simba imefanikiwa
kufika hatua hiyo baada ya kuwa na alama 68 kwenye mechi 29 ambazo
haziwezi kufikiwa na Azam FC yenye alama 52 kwenye mechi 28 wala Yanga
yenye alama 48 kwenye mechi 26.
Kaseja na Kagera Sugar kwa
ujumla wameweza kuitibulia Simba malengo yao ya kuweka rekodi hiyo mbele
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Simba wameweka rekodi ya
kupoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Magufuli aliyehudhuria mechi ya
kwanza katika ligi tangu aingie madarakani.
Tags
SIMBA SC