Yanga imetangaza kufanya mkutano wake mkuu Juni 17 mwaka huu na jina la Tarimba limeonekana kutawala midomoni mwa baadhi ya wanachama wakitaka agombee nafasi hiyo.
“Wana Yanga wakinitaja kuwemo katika wale wanaofikiria wanafaa kuwa viongozi wa klabu kwangu mimi ni heshima kubwa sana na niwashukuru wanayanga kwa kunifikiria hivyo.”
“Niseme nimelisikia na kuliona ni jambo muhimu sana ingawa tunaita ni fitina za kimichezo lakini mimi binafsi nalipa ukubwa sana na ninalifikiria vizuri kwa sababu na mimi ningependa Yanga ifanye vizuri na kama nina weza kutoa mchango kwa klabu yangu kwa nini nisifanye hivyo?
“Kwa kuwa wanayanga wanaona naweza kuchangia kwa namna moja ama nyingine nikiwa kiongozi wao si vibaya kulifikiria. Kama itatangazwa masuala ya uchaguzi nitafikiria sana hili.”
Tags
TARIMBA