BANDA MEDIA BLOG

Disko toto haitaruhusiwa Dar es salaam. - SACP Mambosasa




Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa Kukamata Bastola moja iliosajiliwa kwa namba B86560 mnamo tarehe tano juni mwaka huu, maeneo ya kitunda relini majira ya saa nne wakati askari wakiwa katika doria ambapo waliwakurupusha watu waliokuwa wakijiandaa kwa kufanya uhalifa na mmoja aliangusha silaha hiyo, jeshi nla polisi bado linaendelea na upelelezi ili kugundua mmiliki wa silaha hiyo, Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam SACP. Lazaro Mambosasa leo akizungumza na wanahabari.

Vilevile Kamanda Mambosasa ameendelea kusema kuwa jeshi la polisi linahaimarisha ulinzi na usalama katika kuelekea sikukuu ya Idd el Fitri ambayo inatarajiwa kuwa kesho au kesho kutwa ikiwa ni tamko la Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, na mufti wa tanzania walipokuwa kwenye iftar iliokuwa imeandaliwa na IGP Simon Sirro, jeshi la polisi limeweka mikakati mbalimbali ili kuweka mazingira salama katika sikukuu hiyo.

Hiyo imetokana na viashiria mbalimbali ambavyo hutokea katika misimu ya sikukuu, ambapo kamanda ameongezea kuwa mkoa umepata heshima ya Baraza la Idd kufanyika Dar es salaam kitaifa.

SACP: Mambosasa amesema kuwa jeshi la polisi litatumia pikipiki, Magari, Farasi na askari watakao kuwa kwa mguu katika fukwe za bahari ili kuimarisha ulinzi, vilevile amewataka wananchi kuzingatia kuwa waangalifu kwa kuhakikisha wanakuwa na angalizo la kunywa kwa kiasi na umakini kwa kuepuka vitendo ambavyo vinaweza kuleta uhalifu.

"Disko toto haitaruhusiwa katika kumbi zote katika kanda maalum ya dar es salaam, hatujapata maombi ya yoyote ambayo yameshirikisha jeshi la polisi kukagua ukumbi ulio salama ulioandaliw3a kwaajili ya watoto wadogo hatutegemei mtu yeyote kukusanya watoto kuwarundika bila kuwa na kibali" Mambosasa Amesema

Vilevile Kamanda ametoa wito kwa wazazi kusheherekea sikukuu na watoto wao ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hususani wanapokuwa fukweni ili Kuzuia sikukuu kuzalisha misiba.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG